MSHAMBULIAJI mahiri wa
kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid ameendelea kung'aa sio ndani
ya uwanja lakini hata nje ya uwanja kwa kuwa mchezaji wa kwanza
kufikisha idadi ya mashabiki milioni 100 ambao wame-like ukurasa wake wa
mtandao wa kijamii wa
facebook
. Ronaldo
ambaye ni mshindi mara mbili wa tuzo wa Ballon d'Or msimu huu ameanza
vyema kwani ameshafunga mabao 18 katika mechi 14 za mashindano yote
alizocheza mpaka sasa. Nyota mwingine anayemfuata kwa karibu kwa kuwa na
Likes nyingi katika mtandao huo ni wanamuziki Shakira, Eminem na
Rihanna. Ronaldo alitengeneza video fupi ya kuwashukuru mashabiki wake
popote walipo na kudai kuwa hiyop ni hatua kubwa kwao na
kwake. Wachezaji soka wengine wanaomfuata kwa karibu Ronaldo, ni nyota
wa Barcelona Lionel Messi mwenye idadi ya Likes milioni 74.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni