STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 27 Aprili 2016

KASEKE AING'ARISHA YANGA, MUDATHIR AIZAMISHA MAJIMAJI, VIPORO VIMESALIMIKA....



Mabingwa wa Afrika Mashariki na kati Azam FC wameishusha Simba SC toka katika nafasi ya pili mpaka nafasi ya tatu baada ya leo Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 2-0 mbele ya Majiamaji FC.

Katika mchezo huo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Azam complex Majimaji FC waliuanza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata faulo karibu na lango la Azam FC na kushindwa kuutumia.
Azam FC walianza kukaa sawa katika mchezo kadri ya muda ulivyokuwa unasogea na kuanza kutawala mchezo na kusaka goli la kuongoza.

Azam FC na Majimaji FC walitengeneza nafasi chache walizoshindwa kuzitumia na kupeleka mchezo kwenda mapumziko wakiwa sare ya bila kufungana.


Azam FC walirejea kwa kasi kipindi cha pili na katika dakika ya 50 Mudathir Yahya alimalizia krosi ya Gardiel Michael na kuiandikia Azam FC goli la kuongoza.


Kuingia kwa goli hilo kuliwatuliza Azam FC na kuanza kucheza soka la kuonana huku Majimaji wakijaribu kutenegeneza nafasi za kufunga goli.


Alikuwa Mudathir Yahya tena katika dakika ya 62 akimalizia pasi ya Khamisi Mcha na kuiandikia Azam FC goli la pili na kupeleka mchezo kumalzika kwa Azam FC kubuka na ushindi wa goli 2-0.


Kwa matokeo hayo Azam FC wamefikisha jumla ya pointi ya 58 wakiwa mbele kwa pointi 1 dhidi ya Simba SC wenye pointi 57, na pointi 4 kutoka kwa yanga sc wenye pointi 62.



Kwenye uwnja wa taifa
YANGA SC imetanua wigo wa pointi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mgambo JKT jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe pointi 62 baada ya kucheza mechi 25, ikifuatiwa na Azam FC sasa yenye pointi 58 za mechi 25 pia, wakati Simba SC inaendelea kushika nafasi ya tatu kwa pointi zake 57 za mechi 25.
 
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa kutoka Mwanza, hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, Mgambo wakitangulia na wenyeji Yanga kusawazisha.

Bolly Shaibu aliifungia Mgambo JKT dakika ya nne, akimalizia pasi ya Nassor Gumbo ambaye alimpokonya mpira kiungo wa Yanga, Salum Telela nje kidogo ya boksi baada ya kuanzishiwa na kipa wake, Deo Munishi ‘Dida’.
 
Yanga walionekana kupoteana baada ya bao hilo la mapema na Gumbo akakaribia kufunga bao la pili dakika ya sita kama si juhudi za kipa Dida.
 
Yanga ilipata pigo dakika ya 20, baada ya beki wake tegemeo wa kulia, Juma Abdul kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ikichukuliwa na mkongwe, Mbuyu Twite kutoka DRC. 
 
Kiungo Deus Kaseke akaifungia Yanga bao la kusawazisha dakika ya 43 akimalizia pasi ya kichwa ya Mrundi Amissi Tambwe baada ya krosi nzuri ya juu ya beki wa kushoto, Oscar Joshua.

Almanusra Paul Nonga aifungie Yanga dakika ya 45 baada ya krosi nzuri ya Telela, lakini kichwa cha kudundisha alichopiga kikapaa juu kidogo ya lango.
 
Kipindi cha pili, kocha wa Yanga, Mhoalanz, Hans van der Pluijm alianza kwa mabadiliko, akimpumzisha Nonga na kumuingiza Mzimbabwe Donald Ngoma.
 
Mabadiliko hayo yaliongeza ubora wa Yanga uwanjani dhidi ya wapinzani na dakika ya 53 Ngoma alipiga nje akiwa anatazama nyavu baada ya krosi ya Msuva.
 
Bolly Shaibu alikaribia kufunga dakika ya 60 baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Yanga, lakini kipa Dida alitoka na kupambana naye hadi kumharibia mipango yake.
 
Deus Kaseke tena akawainua vitini wana Yanga dakika ya 72 akimalizia mpira uliookolewa na Bakari Mtama baada ya kichwa cha Tambwe kufutaia krosi nzuri ya Niyonzima.
 
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul/Mbuyu Twite dk20, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Thabani Kamusoko dk72, Paul Nonga/Donald Ngoma dk46, Amissi Tambwe na Deus Kaseke.
 
Mgambo JKT; Said Hamisi, Salum Mlima, Chande Magoja, Henry Chacha, Bakari Mtama, Salum Kipaga, Nassor Gumbo/Ally Nassor ‘Ufudu’ dk79, Mohammed Samatta, Herbert Lukindo, Bolly Shaibu na Salum Aziz Gilla.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox