STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 30 Aprili 2016

YANGA YAWASAMBARATISHA TOTO AFRICANS KIRUMBA.................


Juma Abdul ameihakikishia Yanga SC pointi tatu muhimu hii leo katika uwanja wa CCM Kirumba, ambazo zinawapelekee kuendelea kujikita kilelelni mwa msimamo wa ligi kuu ya vodacom.
VPL-Tanzania  

Katika mchezo huo ambapo Yanga SC walikuwa wageni wa Toto Africans ya Mwanza, ulianza kwa Toto African kutawala mchezo kwa dakika 5, kabla ya kuachja utawala wa mchezo kwa yanga sc.
Katika dakika ya 5 Yanga SC amanusura wapate goli kupitia kwa Saimon Msuva baada ya kupoteza nafasi ya kufunga, na baada ya nafasi hiyo Yanga SC walitengeneza nafasi nyuingine 3 za wazi ambazo walishindwa kuzitumia

Toto African waliandika goli la uongozi katika dakika ya 39 kupitia kwa William Kimanzi akiungo kona ya Abdallah Seseme na kuipeleka Toto African mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili Yanga SC walirejea kwa kasi na katika dakika ya 49 Amisi Tambwe aliisawazishia Yanga SC akimalzia krosi ya Donald Ngoma.

Kuingia kwa goli hilo kuliwaamsha Toto Africans na kuanza kucheza kwa tahadhari kubwa huku Yanga wakiendelea kulisakama lango la Toto Africans.

Katika dakika ya 78 Juma Abdul alimalizia mpira uliotoka kuokolewa na beki wa Toto Africana na kuaindika Yanga goli la pili  na kupeleka mchezo kumalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

Kwa matokeo hayo Yanga inaongeza tofauti ya pointi baina yake na wapinzake wake katika mbio za ubingwa kutoka pointi 4 mpaka pointi 7.


Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Haruna Niyonzima/Thabani Kamusoko, Salum Telela, Simon Msuva, Amissi Tambwe/Malimi Busungu, Donald Ngoma na Deus Kaseke/Matheo Anthony.
 
Toto Africans; Mussa Mohamed, Eric Muliro, Hassan Khatibu, Salum Chukwu, Carlos Protus, Jamal Soud, Abdallah Seseme, Waziri Junior, William Kimanzi na Edward Christopher. 



              MATOKEO YA MICHEZO MINGINE;
2016-04-30






FTAFRICAN SPORT 1 : 0COASTAL UNION
FTMWADUI FC 2 : 1STAND UNITED
FTMTIBWA SUGAR 1 : 0MBEYA CITY
FTT.PRISONS 1 : 1JKT RUVU
                                                   
                                                        MCHEZO UNAOKUJA
2016-05-01
16:00SIMBA SCVs    Azam FC
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox