STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 1 Mei 2016

STORI KUBWA MBILI LEO MEI MOSI KUHUSU MATOKEO YA SIMBA NA HABARI YA YANGA DHIDI YA SAGRADA..






SIMBA SC imelazimisha sare ya bila kufungana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Matokeo hayo yatapokewa kwa furaha na mahasimu, Yanga ambao sasa wanaongoza Ligi Kuu kwa wastani wa pointi sita kuelekea mechi nne za mwisho.

Kwa sare hiyo ya 0-0, Azam FC inafikisha pointi 59, wakati Simba sasa inakuwa na pointi 58, nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 65 baada ya timu zote kucheza mechi 26.





Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mathew Akrama wa Mwanza, aliyesaidiwa na washika vibendera Abdallah Mrisho wa Pwani na Omar Kambangwa wa Dar es Salaam hakukuwa na mashambulizi ya kusisimua na timu zote zilionekana kucheza kwa tahadari kupita kiasi, hivyo kuufanya mchezo upooze.

Lakini kipindi cha pili, kilianza kwa mchezo wa kukamiana na kuchezea rafu na undava, jambo ambalo hata hivyo refa Akrama alilidhibiti kwa busara za kuwatuliza wachezaji wa timu zote mbili kwa kuzungumza nao.


 
Baada ya hapo, kidogo mchezo wenye hadhi ya timu kubwa katika Ligi Kuu ya nchi, tena zinazowania ubingwa ndiyo ukaanza kuonekana kwa mshambulizi ya pande zote mbili.

Nahodha wa Azam FC, John Bocco peke yake akakosa mabao mawili ya wazi na kushika kichwa kwa masikitiko, wakati upande wa Simba Hamisi Kiiza na Hajji Ugando walipoteza pia nafasi za wazi.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Emery Nimubona, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid/Brian Majwega dk74, Novart Lufunga, Justise Majabvi, Awadh Juma, Jonas Mkude, Hamisi Kiiza, Danny Lyanga/Hajji Ugando dk54 na Peter Mwalyanzi.

Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Aggrey Morris, David Mwantika, Jean Mugiraneza/Kipre Balou dk76, Ramadhani Singano ‘Messi’/Mudathir Yahya dk46, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Kipre Tchetche/Ame Ali ‘Zungu’ dk65, John Bocco na Khamis Mcha ‘Vialli’.



MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM

RnTimuPWDLFAGdPts
1YANGA26205161154665
2Azam FC26178143162759
3SIMBA SC26184443142958
4MTIBWA SUGAR27137730191146
5T. PRISONS27101252422242
6MWADUI FC27107102726137
7STAND UNITED26104122324-134
8NDANDA FC2771282627-133
9MAJIMAJI FC2796122036-1633
10MBEYA CITY2786132834-630
11TOTO AFRICANS2879122638-1230
12AFRICAN SPORT2875161230-1826
13JKT RUVU2667132535-1025
14KAGERA SUGAR2767141931-1225
15MGAMBO SHOOTING2758142134-1323
16Coastal Union2857161638-2222



……………………….

                                   STORI YA PILI;

 
MAREFA kutoka nchini Madagascar watachezesha mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati Sagrada Esperanca na Yanga SC ya Tanzania Mei 17, mwaka huu Uwanja wa Sagrada Esperanca, zamani Quintalao do Dundo.

 

 


Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) marefa hao ni Hamada el Moussa Nampiandraza atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Velomanana Ferdinand Jinoro na Jean Thierry Djaonirina.



Hata hivyo, CAF bado haijateua marefa wa kuchezesha mechi ya kwanza baina ya timu hizo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Mei 7. 



 


Yanga imeangukia katika kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Shirikisho, baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2, ikilazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam na kufungwa 2-1 Alexandria.



Yanga ilianza vizuri tu kwa kuzitoa Cercle de Joachim ya Mauritius kwa jumla ya mabao 3-0, ikishinda 1-0 ugenini na 2-0 nyumbani kabla ya kuitoa na APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 2-1 Kigali na kutoa sare ya 1-1 Dar es Salaam.

 
Kwa upande wao, Sagrada Esperanca katika Raundi ya Awali waliitoa Ajax Cape Town ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya kufungwa 2-1 ugenini na kushinda 2-0 nyumbani. 


Katika Raundi ya kwanza wakaitoa LD Maputo ya Msumbiji kwa jumla ya mabao 2-1 ikishinda 1-0 nyumbani na kutoa sare ya 1-1 ugenini na kwenda hatua ya 16 Bora, ambako waliitoa V. Club Mokanda ya Kongo kwa jumla ya mabao 4-1 wakishinda 2-1 ugenini na 2-0 nyumbani.
……………………

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox