STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 1 Desemba 2014

THIERRY HENRY ATUNGIKA DALUGA MAREKANI, APANIA KURUDI KIVINGINE ARSENAL

MSHAMBULIAJI Thierry Henry ametangaza kuondoka klabu ya New York Red Bulls ya Marekani baada ya kuitumikia kwa miaka minne na nusu katika Ligi Kuu ya nchini humo.
Mwanasoka huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, ametangaza uamuzi wake huo siku tatu baada ya kukiri anapenda kurudi Arsenal, na kubadilisha picha yake ya bango katika ukurasa wake wa Facebook kwa kuweka picha ya Uwanja wa Emirates.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 37 atatumia wiki chache zijazo kuamua mustakabali wake wa baadaye wa maisha, huku kufundisha klabu katika Ligi Kuu ya England ikiwa moja ya mipango.
Thierry Henry, pictured celebrating scoring in January 2012, admitted he would love to return to Arsenal
Thierry Henry, pichani akishangilia bao Januari mwaka 2012, amesema angependa kurejea Arsenal

MATAJI YA THIERRY HENRY NA KLABU ALIZOCHEZEA

1994-1999: Monaco (Mechi 105, mabao 20)
1999-1999: Juventus (Mechi 16, mabao 3)
1999-2007: Arsenal (Mechi 254, mabao 174)
2007-2010: Barcelona (Mechi 80, mabao 35)
2010-2014: New York Red Bulls (Mechi 122, mabao 51)
2012-2012: Arsenal (mkopo) (Mechi 4, bao 1) 
1997-2010: Ufaransa (Mechi 123, mabao 51)
Monaco: Ligue 1, Taji la ubingwa 
Arsenal: Ligi Kuu (2), Kombe la FA (3), Ngao ya Jamii (2)
Barcelona: La Liga (2), Kombe la Mfalme, Super Cup ya Hispania, Ligi ya Mabingwa, Super Cup ya Ulaya, Klabu Bingwa ya Dunia
New York Red Bulls: MLS Kanda ya Mashariki (2), Ngao ya Mashabiki 
Ufaransa: 1998 Kombe la Dunia, Euro 2000, Kombe la Mabara 2003
Henry changed his cover photo on Facebook to an image of the Emirates following his announcement
Henry amebadilisha picha yake ya bango Facebook na kuweka ya Uwanja wa Emirates 

"Nachukua fursa hii kutangaza kwamba kwa bahati mbaya Jumamosi ilikuwa mechi yangu ya mwisho kwa New York Red Bulls," Henry amesema leo.
Henry aliliambia jarida la L'Equipe la Ufaransa Ijumaa kwamba atabakia kwenye soka baada ya kustaafu kama mchezaji kwa kugeukia ukocha, ushauri au utendaji.
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwaka 1998 amekiri kujuta kushindwa kuisaidia Arsenal kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na ndiyo maana anataka kwenda kutoa mchango wake katika klabu ipate mafanikio Ulaya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox