STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 1 Desemba 2014

VAN GAAL ACHUKIZWA NA RATIBA YA LIGI KUU KIPINDI CHA KRISMASI.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal ameonyesha kutofurahishwa na ratiba ya Ligi Kuu itakavyokuwa katika kipindi cha sikukuu za krismasi na mwaka mpya. Kuna uwezekano mkubwa United ikacheza mechi nne ndani ya siku tisa katika kipindi cha kati ya Desemba 29 mpaka Januari 3 kutegemeana na ratiba ya Kombe la FA itakavyokuwa. Ratiba katika Ligi Kuu inaonyesha kuwa watakuwa wenyeji wa Newcastle United Desemba 26, kabla ya kucheza wa ugenini dhidi ya tottenham Hotspurs siku mbili baadae na siku ya mwaka mpya watapepetana na Stoke City. Akihojiwa Van Gaal amesema ana mke, watoto na wajukuu na hawezi kuwaona katika kipindi cha krismasi lakini alitaka kufanya kazi katika Ligi Kuu hivyo anapaswa kuzoea hali iliyopo. Van Gaal amesema hafurahishwi na suala hilo lakini hawezi kubadilisha na hadhani kama ni jambo zuri kwa wachezaji pia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox