Nguli
wa Arsenal Jens Lehmann amemsisitiza Petr Cech kufurahia msimu bora
kabisa katika klabu ya Arsenal, lakini amemuasa kuwa anahitaji muda
kuweza kuzoea maisha mapya klabuni hapo kufuatia uhamisho wake kutoka
Chelsea.
Cech
alifanya makosa ya kizembe ambayo yaliigharimu Arsenal kupoteza mchezo
wake wa kwanza wa ligi kwa mabao 2-0 dhidi ya West Ham uliopigwa
Jumapili katika dimba la Emirates huku ukiwa ndio mchezo wake kwanza wa
ligi akiwa ndani ya uzi wa Arsenal.
Lehmann,
ambaye alikuwa katikati ya lango katika kikosi cha Arsenal kilichotwaa
ndoo ya EPL bila ya kufungwa msimu wa 2004, amekiri kushtushwa na
kiwango cha Cech lakini anaamini kwamba mlinda mlango huyo atakuja
kivingine na kuonesha yale aliyokuwa akiyafanya pindi alipokuwa Chelsea.
"Nimeshangazwa
kwa sababu nilitarajia kuona akionesha kiwango kikubwa punde tu msimu
unapoanza”, Lehmann alikaririwa na mtandao wa Goal kutoka Marekani.
"Lakini
wakati mwingine inachua muda kidogo kuzoea mazingira mapya, hasa
unapotoka kwa mahasimu wako wakubwa kama Chelsea. Huchukua muda kwa
kweli, cha msingi anatakiwa kusahau yote hayo.
"Ni
aina ya makipa ambao Arsenal walikuwa wakihitaji ili kutwaa ubingwa",
Lehmann aliongeza. "Ana uzoefu wa kutosha, yaani ana sifa zote za kuwa
mlinda mlango bora na naweza kusema ni miongoni mwa walinda mlango bora
kabisa ulimwenguni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni