STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 13 Agosti 2015

MAJABVI AANGUKA MIAKA MIWILI SIMBA SC, AVEVA AGAWA ZAWADI KWA MASHABIKI

KLABU ya Simba jana usiku ilimsainisha kiungo mkabaji wa kimataifa kutoka Zimbabwe, Justice Majabvi, mkataba wa miaka miwili wa kuichezea timu hiyo inayojiandaa kushiriki msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ambao utafanyika kuanzia Septemba 12 mwaka huu.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo, Haji Manara,alisema kuwa mchezaji huyo alipewa mkataba baada ya Kocha Mkuu, Muingereza, Dylan Kerr, na benchi la ufundi kuridhishwa na kiwango cha mchezaji huyo.

Manara alisema kwamba bado benchi la ufundi linaendelea kusaka mchezaji mmoja wa nafasi ya ushambuliaji ambaye atakamilisha usajili wa Simba na kusubiri kuanza kwa msimu mpya wa ligi.
Msemaji wa Simba SC, Hajji Manara (kulia) akimshuhudia Justuce Majabvi akisaini Mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo

"Msimu huu hakuna mchezaji atakayesainiwa Simba kama hajapitishwa na benchi la ufundi, hii ni kutaka kuondoa ile misemo kwamba viongozi wanasajili wachezaji na kuingilia majukumu ya kocha", alisema Manara.
Wakati huo huo, Rais wa Simba, Evans Aveva, jana alisema kuwa klabu hiyo haijamuacha kipa wao mkongwe, Ivo Mapunda, ila kipa huyo ndiye alikataa kusaini mkataba ambao amepewa.
Hata hivyo habari zilizopatikana jijini zinaeleza kuwa Mapunda alikataa kusaini mkataba huo mpya baada ya ule wa mwaka mmoja aliokuwa nao kumalizika, kutokana na kutakiwa kusaini bure.
Aveva alisema pia hadi jana viongozi wa Simba walikuwa hawajafikia maamuzi ya kuendelea au kumuacha mshambuliaji, Elias Maguli, ambaye hakuwa kwenye kikosi cha wachezaji 20 wa Kerr waliotajwa kujiandaa na mchezo wa Simba Day.
Rais wa Simba Evans Aveva, Mkurugenzi wa kampuni ya EAG Ggroup Limited Imani Kajula na Msemaji mkuu wa klabu ya Simba Haji Manara wakipiga picha ya pamoja na washindi bahati nasibu siku ya Simba Day.‏ 

Mwandishi wa habari ambaye aliweza kujishindia bahati nasibu ilichezeshwa leo katika mkutano na waandishi wa habari‏

Wakati huo huo: Simba leo imekabidhi zawadi za simu na jezi kwa wanachama wake walioshinda katika bahati nasibu iliyochezeshwa baada ya kukata tiketi kuingia uwanjani siku ya Simba Day.
Akikabidhi zawadi hizo, Rais wa Simba, amesema kwamba lengo la kutoa zawadi hizo ni kuthamini mchango wa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo waliojitokeza siku ya tamasha hilo.
Aveva pia aliwashukuru wanachama na mashabiki wote waliohudhuria Simba Day na kueleza kwamba tamasha la mwaka huu lilifana kuliko matamasha mengine yaliyotangulia tangu waanzishe utaratibu huo.
"Pia tunashukuru kwa kufanikisha Simba Week nayo ilifanyika kama ilivyopangwa", alisema Aveva.
Rais huyo pia aligawa mipira tisa kwa shule tatu za hapa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuendeleza soka la vijana na utaratibu huo wanatarajia kuufanya watakapotembelea mikoani.
"Lengo letu ni kuanza kutunza vipaji vya watoto, tumeanza na Dar es Salaam na tutaanzisha Simba Cup", aliongeza kiongozi huyo.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG, Imani Kajula, alisema kuwa mashabiki wa timu hiyo wanatakiwa kuendelea kununua jezi rasmi zilizotambulishwa ili kuiingizia klabu mapato.
Alisema kwamba utaratibu wa kununua kwa njia ya mtandao ni rahisi na unafanya mteja kuletewa popote alipo kama yanavyofanya maduka makubwa duniani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox