STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 22 Juni 2014

RAIS WA CHUO CHA BUGANDO ALIYEPOTEA TOKA TAR 18 MWEZI HUU APATIKANA AKIWA KAPOTEZA FAHAMU MAENEO YA USAGARA

Bw.Mussa Leonard Mdede Aliyesimama.
 
Rais wa chuo kikuu cha CUHAS (Bugando) na Mwenyekiti wa Shirikisho la wanafunzi vyuo vikuu nchini (TAHLISO), Bw.Mussa Leonard Mdede ameokotwa usiku huu  katika maeneo ya Usagara nje kidogo ya jiji la Mwanza, akiwa amepoteza fahamu (hajitambui)  lakini hana majeraha yoyote na amepelekwa katika hospitali ya rufaa Bugando kwa ajili ya vipimo na kupatiwa matibabu.
 
Kwa sasa ameweza kuongea (japo kwa taabu) lakini hakumbuki chochote kilichotokea.
 
Bw.Mdede alitoweka ghafla siku ya jumatano tar.18 mwezi huu, saa kumi jioni,na haikuweza kufahamika mara moja yupo wapi, mpaka usiku huu taarifa za kupatikana kwake zilipotolewa.
 
Taarifa hizi zimedhibitishwa na Waziri Mkuu wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo, Bw.Benjamin Thomas. Taarifa zaidi juu ya hali ya Bw.Mdede zitazidi kutolewa kwa kadri zinavyopatikana.
 
 Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mwanza ameahidi kutoa taarifa leo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox