CHAMA cha Soka nchini
Uingereza, FA kina uhakika kuwa Uwanja wa Wembley una nafasi kuandaa
fainali ya michuano ya Ulaya 2020 na pia hawajatoa uwezekano wa kuandaa
michuano hiyo mwaka 2028.
Katibu Mkuu wa FA Alex horne ana matumaini
uwanja huo wa taifa wa Uingereza unaweza kuandaa mchezo wa nusu fainali
na fainali katika kipindi cha miaka sita ijayo.
Uwanja wa Allianz Arena
uliopo jijini Munich ndio uwanja mwingine pekee unaogombani nafasi hiyo
na Hornes anafikiri nafasi yao inaongezeka kutokana na Ujerumani kutilia
mkazo nafasi yao ya kuandaa michuano ya Ulaya mwaka 2024. Michuano ya
Ulaya mwaka 2020 itaandaliwa katika miji 13 tofauti huku mchezo wa
fainali na nusu fainali ukiandaliwa katika uwanja mmoja huku miji
iliyoshinda kupata nafasi hiyo ikitarajiwa kutangazwa Septemba 19 mwaka
huu. Mara ya mwisho Uingereza kuandaa michuano mikubwa ya soka ilikuwa
ni mwaka 1996 walipoandaa michuano ya Ulaya huku pia wakiwa wamewahi
kuandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1966.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni