STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 12 Septemba 2014

DIEGO COSTA MCHEZAJI BORA WA MWEZI ENGLAND, KOCHA SWANSEA AANGUSHA VIGOGO

 
Diego Costa ndiye mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya England baada ya kazi nzuri Chelsea
MSHAMBULIAJI Diego Costa ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Agosti wa Ligi Kuu ya England.
Mpachika mabao huyo wa Chelsea amefunga mabao manne katika mechi tatu za mwanzo wake wa kuhamia LIgi Kuu ya England akiwa na Chelsea.
Aidha, baada ya mwanzo mzuri akiwa na Swansea, Garry Monk ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi huo baada ya kuiwezesha timu yake kushinda mechi zake zote tatu, ikiwemo dhidi ya Manchester United Uwanja wa Old Trafford.
Garry Monk ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi baada ya kuiwezesha Swansea kushinda mechi zote tatu za mwanzo

WALIOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AGOSTI LIGI KUU ENGLAND;

Diego Costa (Chelsea) 
Cesc Fabregas (Chelsea)
Nathan Dyer (Swansea)
Gylfi Sigurdsson (Swansea)
Andreas Weimann (Aston Villa) 
Costa amefanikiwa kuhamishia cheche zake za La Liga katika Ligi Kuu ya England baada ya kutua Chelsea kufuatia kocha Jose Mourinho kumsajili nyota huyo kwa Pauni Miliomi 32 kutoka Atletico Madrid.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Hispania alifunga katika mechi yake ya kwanza kwenye ligi hiyo dhidi ya Burnley na akarudia tena kufunga dhidi ya Leicester, kabla ya kufunga mavao mawili katika ushindi wa 6-3 dhidi ya Everton.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox