STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 11 Septemba 2014

GARY NEVILLE AISHAMBULIA SERA YA USAJILI YA MANCHESTER UNITED, ASEMA KUMUUZA WELBECK ARSENAL NI AJABU

Manchester United sold Danny Welbeck to rivals Arsenal for £16million after the arrival of Radamel Falcao
Manchester United walimuuza Danny Welbeck kwa wapinzani wao wakubwa Arsenal baada ya kumsaini Radamel Falcao.

GARY Neville ameishutumu sera ya usajili ya Manchester United baada ya kudai kuwa alishangazwa na kitendo cha kumuuza Danny Welbeck kwa paundi milioni 16 tu.
United walitumia fedha nyingi majira ya kiangazi kwa kumsajili Falcao, Angel di Maria, Daley Blind, Ander Herrera, Luke Shaw na Marco Rojo.
Neville alisema: "Sikutarajia kama United wangefanya biashara kama hiyo, nalidhani wangefanya zaidi ya hapo"
"Siwezi kusema sana, wiki iliyopita nilifanya kazi na Danny Welbeck  (akiwa na England), hakika ni ajabu. Nakiri wazi kuwa kumuuza Danny Welbeck ni ajabu, lakini ni kwa upande wangu".
"Kwa pesa zote walizotumia majira ya kiangazi, kuna mabeki wa kushoto na kulia walionunuliwa kwa paundi milioni 14, 16, 16?
"Arsenal walimpaje Welbeck kwa paundi milioni 16? Sielewi. Wamewasaidia wapinzani kwasababu Arsenal watakuwa wanapambana kusaka nafasi nne za juu"
"Napata shida kupata logiki, lakini sielewi, inashangaza kwa namna moja ama nyingine".
"Falcao aliingia pale, ilimshangaza kila mtu. Inaingiaje kwenye timu, sijui. Tayari walikuwa na  Rooney, Di Maria, Robin van Persie, Falcao, Herrera, Januzaj na Mata  katika timu.
Arsene Wenger alimsajili  Danny Welbeck baada ya mshambuliaji wake chaguo la kwanza Olivier Giroud kuumia
Radamel Falcao alijiunga Manchester United kwa mkopo wa Muda mrefu.

Neville aliendelea kudai kuwa United imelipa hela nyingi zaidi kwa wachezaji baada ya kushika nafasi ya saba msimu uliopita.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox