KLABU
ya Manchester City imetoa jezi mpya za tatu zitakazotumiwa na mabingwa
hao wa Ligi Kuu ya England katika michuano ambayo watashiriki msimu huu.
Klabu
hiyo inazindua jezi hizo kuelekea kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi
ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich Jumatano na zitatolewa rasmi
kwa ajili ya mashabiki kuanzia Septemba 25.
Taarifa
ya City kwa vyombo vya habari, imesema: "Chini ya wingu la kiza hizi
jezi zinaonekana zinawaka, kama zinatiwa nguvu ya betri na zitatoa
mwangaza fulani wa rangi uwanjani,".
Hii ndiyo jezi kamili mpya ya tatu ya Man City
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni