STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 16 Desemba 2014

SIMBA SC YAMWONGEZA OKWI MWAKA MMOJA MSIMBAZI

Klabu ya Simba imemuongeza kiungo mshambuliaji Mganda Emanuel Okwi mkataba wa mwaka mmoja baada ya ule wa miezi sita kukaribia ukingoni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uteandaji ya Simba SC, Zacharia Hanspope amethibitisha muda mfupi uliopita juu ya usajili huo na kuweka wazi kwamba wameamua kumwongeza kandarasi hiyo nyota huyo baada ya kuona mchango wake katika kikosi chao.
“Okwi ni mchezaji mzuri, amekuwa akifanya kazi nzuri katika kikosi chetu. Leo tumemuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja,” amesema Hanspope.
okwii
Okwi aliyezaliwa Desemba 25, 1992, amesaini mkataba huo mbele ya Rais wa Simba SC, Evans Aveva.
Okwi alijiunga na Simba SC kwa mkataba mfupi wa miezi sita Agosti mwaka huu ili kulinda kiwango chake wakati akiendelea na kesi iliyokuwa ikimkabili dhidi ya Yanga SC. Mganda huyo alishinda kesi hiyo baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuthibitisha kwamba mkataba wake na Yanga SC ulikuwa umevunjwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox