STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 12 Januari 2015

MESSI, RONALDO, NEUER NANI KUSHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA DUNIA LEO

ORODHA ya mwisho ya wachezaji watatu wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa dunia FIFA Ballon d'Or inayofanyika leo jumatatu mjini Zurich, Uswizi, wametangazwa ambao ni Lionel Messi, Manuel Neuer na Cristiano Ronaldo.
Hizi ni takwimu zinazowafanya Ronaldo na Messi waingie katika kinya’anyiro cha mwisho kwa mwaka 2014.
Messi: Baada ya kufunga goli moja katika fainali za kombe la dunia zilizopita (2010), Lionel Messi alifunga mabao manne katika fainali za mwaka 2014 na kushinda kiatu cha mchezaji bora wa mashindano. Alikuwa na magoli 52 katika mechi 62 za klabu na nchi yake, pia akiongeza ya La Liga na UEFA aliyofunga mwezi uliopita.
Cristiano Ronaldo: Alishinda tuzo iliyopita ya Ballon d'Or, alifunga magoli 69 katika mechi 59 za Real Madrid na Ureno mwaka 2013. Akiwa na mabao 55 katika mechi 55 mwaka huu ni rekodi kali, ingawa mabao yake 45 katika ligi na mashindano ya ulaya ni magoli sita zaidi ya mchezaji yeyote aliyefunga katika michuano ya mwaka huu katika ligi tano za juu. Pia aliweka rekodi ya kufunga magoli mengi zaidi katika msimu mmoja wa UEFA, akifunga magoli 17 katika msimu wa 2013-14.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox