STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 6 Agosti 2015

MKWASA ATANGAZA KIKOSI KICHOIVAA NIGERIA, AZAM YAZIPIKU SIMBA NA YANGA


BAADA ya kuisaidia timu yake ya Azam FC kutwaa kombe la Kagame 2015, Farid Mussa pamoja na wachezaji wenzake nane wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ chenye wachezaji 29 kitakachocheza na Nigeria.
Awali akitangaza kikosi hicho ambacho kitaingia kambini jumapili, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface, aliweka wazi kuwa wameangalia wachezaji kwenye mashindano ya Kagame, ambayo yamemalizika hivi karibuni.
Kikosi hiki cha wachezaji 29 wataingia kambini siku ya Jumapili katika hoteli ya Tansoma iliyopo Gerezani kwa ajili ya kambi ya wiki moja ya mazoezi kabla ya kwenda kuweka kambi ya siku kumi jijini Istambul - Uturuki, ambapo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za Taifa za Libya na Kuwait kabla ya kurejea nchini kuwavaa Nigeria”, alisema Mkwassa
Katika kikosi hicho Mkwasa amewajumuisha wachezaji watano wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi (Proffesional), ambao baadae watajumuika kwa kambi ya kujiandaa kucheza na Nigeria, Septemba 2015 nchini Uturuki.
Katika kikosi hicho klabu ya ndio imeongoza kutoa wachezaji wengi, ambapo Azam FC wachezaji tisa, Yanga wachezaji ni saba, Simba wameitwa wachezaji watatu huku Mwadui FC, Ruvu Shooting na Mafunzo zikiwatoa mchezaji mmoja mmoja.
Wachezaji walioitwa ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga SC) na Aishi Manula (Azam FC), walinzi wa pembeni: Shomari Kapombe (Azam FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Juma Abdul, Mwinyi Haji (Yanga SC) na Abdi Banda (Simba SC).
Walinzi wa kati; Hassan Isihaka (Simba SC), Nadir Haroub, Kelvin Yondani (Yanga SC), Viungo wakabaji: Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Viungo washambuliaji ni Salum Telela (Yanga SC) na Said Ndemla (Simba SC).
Washambuliaji wa pembeni; Orgenes Mollel (Aspire – Senegal), Abdrahman Mbambi (Mafunzo), Deus Kaseke, Saimon Msuva (Yanga SC), Ramdhani Singano, Farid Musa (Azam FC), huku washambuliaji wa kati wakiwa ni John Bocco, Ame Ally (Azam FC) na Rashid Mandawa (Mwadui FC).
Wachezaji wa kimataifa waliojumuishwa katika kikosi hicho ambacho Agosti 23 kitaelekea kambini nchini Uturuki kwa kambi ya siku kumi ni Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – DR Congo), Mrisho Ngasa (Free State - Afrika Kusini) na Hassan Sembi (Santos FC – Afrika Kusini) na Adi Yussuf (Mansfield Town – Uingereza

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox