STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 4 Agosti 2015

USAJILI LIGI KUU ENGLAND WATUMIA PAUNDI MILIONI 500 MPAKA SASA.

KIASI cha paundi milioni 500 zimetumika kwenye usajili wa Ligi Kuu katika kipindi hiki cha kiangazi, pungufu ya paundi milioni 335 zilizotumika kiangazi mwaka jana huku zikiwa zimebaki wiki nne kabla ya dirisha la usajili halijafungwa. 

Uhamisho wa Raheem Sterling kutoka Liverpool kwenda Manchester City kwa kitita cha paundi milioni 44 ndio usajili mkubwa kufanywa mpaka sasa. 

Meneja wa Manachester United Louis van Gaal amedokeza kufanya usajili wa kushangaza pamoja na kutumia paundi milioni 83 mpaka sasa. 

Kuanzia msimu wa 2016-2017 haki za matangazo ya kuonyesha mechi za Ligi Kuu imepanda kutoka paundi bilioni 3.018 mpaka paundi bilioni 5.136 kwa msimu mitatu. 

Kupata huko kwa mapato hayo kunafanya klabu itakayoburuta mkia katika Ligi Kuu kukunja kitita cha paundi milioni 99 kwa msimu huku bingwa akipata zaidi ya paundi milioni 150.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox