Jorge Mendes sio jina geni masikioni mwa wapenda soka wengi duniani, hususani watu wanaofuatilia soka la Ulaya katika nchi kama za Hispania, Ufaransa, Italia na Uingereza, Jorge Mendes ambaye ni wakala wa wachezaji kadhaa wakubwa barani Ulaya akiwemo Cristiano Ronaldo anatajwa na jarida la Forbes kama wakala mwenye nguvu katika soka kwa mwaka 2015.
Jorge Mendes ametajwa na jarida la Forbes
kushika nafasi ya pili katika mawakala ambao wana nguvu ya ushawishi wa
kufanya uhamisho ufanyike katika michezo, akiwa nyuma ya wakala wa
mchezo wa Baseball Scott Boras. Jarida la Forbes limemtaja Mendes kufanya uhamisho wa jumla ya dola milioni 950, ambapo yeye amepata kiasi cha dola milioni 95.
Jorge Mendes ametajwa kuwahi kusimamia dili za uhamisho za wachezaji kadhaa akiwemo Cristiano Ronaldo, Angel Di Maria, David de Gea na Radamel Falcao. Mendes amekuwa akisimamia uhamisho wa wachezaji mbalimbali katika kipindi cha zaidi ya miaka 10 sasa.
Jorge Mendes amesimamia usajili wa Anthony Martial, Angel Di Maria na Nicolas Otamendi katika dirisha la usajili la mwezi August mwaka huu, lakini ni wakala aliyesimamia uhamisho wa pound milioni 80 wa Cristiano Ronaldo kutoka Man United kwenda Real Madrid.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni