Katika umri wa miaka 19 Martial
ameshafunga magoli 5 katika mechi 9, huku katika umri huo huo ilimchukua
Cristiano Ronaldo mechi 39 kufunga magoli hayo 5.
Kijana Huyo raia wa Ufaransa
amekua na mwanzo mzuri huku akimudu presha iliyopo Old Trafford sanjari
na dau kubwa sana alilosajiliwa akitokea Monaco ya Ufaransa.
Anthony Martial alitua Old
Trafford akiwa hafahamiki hadi na nahodha wa klabu hiyo Wayne Rooney,
lakini hadi sasa amekua miongoni mwa wachezaji tegemezi klabuni
akiwapiku hata akina Memphis Depay ambao wana majina makubwa zaidi yake.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni