Mshambuliaji wa Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza Wayne Rooney siku ya jana katika uwanja wa Wembley kwenye mchezo wa Uingereza dhidi ya Estonia alikabidhiwa tuzo ya kiatu cha dhahabu na gwiji wa soka nchini Uingereza Sir Bobby Charlton baada ya kuvunja rekodi yake ya ufungaji wa muda wote kwenye timu ya Taifa.
Sir Bobby Charlton aliichezea timu ya taifa ya Uingereza kwanzia 1958-1970 katika michezo 106 akibahatika kufunga magoli 49 na kuwa mfungaji wa muda wote wa taifa hilo kabla ya Rooney kuvunja rekodi hiyo katika mchezo dhidi ya Switzerland ndani ya dimba la Wembley.
Katika mchezo wa kufuzu Euro 2016 ,Rooney alifunga katika dakika ya 84 na kufikisha magoli 50, moja zaidi ya magoli 49 ya Sir Bobby Charlton.
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/09/wayne-rooney-avunja-rekodi-ya-miaka-45.html
Copyright © saluti5
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/09/wayne-rooney-avunja-rekodi-ya-miaka-45.html
Copyright © saluti5
Sir Bobby Charlton akiwa na Wayne Rooney baada ya kumpatia kiatu cha dhahabu
Sir Bobby Charlton akimkabidhi Wayne Rooney kiatu cha dhahabu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni