STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 22 Oktoba 2015

UCHOYO WA PASI WA MORATA WAMUUDHI POGBA.

KIUNGO wa Juventus, Paul Pogba amekiri kukasirishwa na mchezaji mwenzake Alvaro Morata kwa kushindwa kumpa pasi katka mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Monchengladbach uliomalizika kwa sare ya bila kufungana. 
 
Pogba alikaribia kuipatia bao Juventus katika mchezo huo ulofanyika jijini Turin kwa mpira wa adhabu ambayo iliokolewa vyema na golikipa Yann Sommer na alipata nafasi nyingine nzuri ya kufunga kama Morata angempatia pasi badala ya kujaribu kupiga mwenyewe. 
 
Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Pogba amesema alikasirishwa na Morata na anatumaini katika mechi nyingine atampasia mpira katika eneo muhimu kama lile. 
 
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Barcelona na Chelsea, amefunga bao moja pekee msimu huu lakini amesisitiza kuwa atarejea katika kiwango chake cha juu hivi karibuni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox