STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 29 Machi 2016

HIKI NDICHO KINACHOTAKIWA KUFANYIKA ILI TAIFA STARS ISONGE MBELE AFCON 2017


TAIFA  la wanamichezo limezizima baada ya kusikia taarifa za timu ya taifa ya Chad kujiondoa katika michuano ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (Afcon) ambazo zitafanyika mwakani nchini Gabon.

Kama tunavyofahamu, soka letu hapa barani Afrika limejaa changamoto nyingi sana ikiwemo ya fedha na hii inatokana na nchi nyingi kutokuwa na uchumi mzuri kama ambavyo taifa la Chad limekuwa katika wakati mgumu kwa hivi sasa kutokana na hali mbaya ya kifedha katika serikali yao na kupelekea timu yao ya taifa kushindwa kusafiri kuja Tanzania kwenye mchezo wa marejeano na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa stars.
 https://i.onthe.io/vllkyt7t17ct93moi.bfb1700b.jpg
Baada ya taarifa hiyo wanamichezo wengi wa Tanzania wameonekana kusononeka sana kwa maana matokeo ya ushindi waliyoyapata nchidi Chad siku chache nyuma yamefutwa ingawa pia matokeo ya Misri na Nigeria waliyoyapata mbele ya Chad nayo yamefutwa.

Kwa hali ilivyo mpaka sasa katika Kundi G ambalo ndiyo tukio hilo limetokea, Tanzania ni ngumu kwao kupita lakini pia ni nyepesi kwao kupita. Tizama msimamo ulivyo mpaka sasa.

                  P    W   D    L     GF  GA  GD  Pts
1. Egypt       2    1    1    0    4    1    3    4
2. Nigeria     2    0    2    0    1    1    0    2
3. Tanzania   2    0    1    1    0    3    -3   1

KWA NINI NI NGUMU;
Ngumu kwa Tanzania kwa maana sasa watakabiliwa na michezo miwili migumu dhidi ya Misri na Nigeria michezo ambayo itahitajika ushindi. Misri watakuja Tanzania na kisha Tanzania kwenda Nigeria.

Kwa hali ya vikosi vya timu zote, Tanzania inaonekana kutokuwa na kikosi chenye wapambanaji wengi ukilinganisha na wapinzani wao waliobaki.

Baada ya Chad kujitoa kumelifanya Kundi G kuwa gumu zaidi kwa timu zote za kundi hilo kwa sababu kila timu imeathiriwa na kujitoa kwa Chad. Misri wapo kileleni kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya Nigeria lakini tofauti ya pointi tatu dhidi ya Tanzania.

Mchezo wa Misri dhidi ya Nigeria ni mchezo ambao utakuwa na ushindani mkubwa sana na ni mchezo ambao utatupa matumaini Watanzania.

Endapo Nigeria ikimfunga Misri, itafikisha pointi tano na kukaa kileleni huku Misri ikibaki na pointi zake nne na Tanzania pointi moja, hivyo itafanya mchezo wa Stars dhidi ya Nigeria kuwa mgumu zaidi kwa maana Nigeria ikishinda itafikisha pointi nane ambazo zitamfanya afuzu kama kinara wa kundi, haitajalisha matokeo ya Stars na Misri, wakati huo Stars kama nayo ikimfunga Nigeria na Misri, basi itafuzu kwa pointi saba.

Na kwa upande wa Misri, endapo ikishinda mchezo wake dhidi ya Nigeria itamfanya kuwa na asilimia 98 za kufuzu kwa maana itafikisha pointi saba, pointi ambazo zitamfanya Nigeria aondolewe katika kinyang’anyiro cha kuwania kufuzu na wakati huo itatakiwa Stars imfunge Nigeria pamoja na Misri kwa idadi kubwa ya mabao ili mwisho wa siku Stars impige gepu Misri kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa baada ya wote kuwa na pointi saba.

Pia kama Misri na Nigeria zikitoka sare, itakuwa neema zaidi kwa Watanzania kwa sababu Misri itafikisha pointi tano na Nigeria tatu, hivyo Tanzania ambayo itacheza nao wote hawa itahitajika ishinde mechi zote hizo kwa idadi yoyote ya mabao ili afikishe pointi saba na kufuzu bial ubishi.

Kwa maana hiyo, kimahesabu nafasi kubwa kwa Tanzania ni kuwaombea Nigeria washinde dhidi ya Misri au walazimishe sare leo usiku ili na sisi tujipange vyema kimapambano tuchukue pointi zote sita kwa mataifa hayo kisha tufuzu kwa mara ya pili kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox