STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 15 Machi 2016

MATOKEO NA REKODI KATIKA MICHEZO YA JANA UEFA CHAMPIONS LIGI...............

 Manchester City 0-0 Dynamo Kiev (3-1 agg): Hosts confirm quarter-final spot but captain

Manchester City wamefanikiwa kufuzu kucheza robo fainali ya michuano ya Champions League  kwa mara ya kwanza licha ya kutoka sulusu kwenye mchezo wao wa marudiano dhidi ya Dynamo Kiev jana usiku.

City ilishinda kwa bao 3-1 kwenye mchezo wa awali, walianza vyema mchezo huo lakini wakajikuta wakiwakosa walinzi wao nguzo wa kati Vincent Kompany na Nicolas Otamendi dakika za mapema baada  ya kuanza kwa mchezo huo kutokana na kupata majeraha na kushindwa kuendelea na mchezo.
City-rekodi 1

Hadi kipindi cha kwanza inamalizika hakuna timu ambayo ilikuwa imepiga hata shuti moja on target. Jesus Navas alipiga shuti ambalo liligonga mwamba wakati shuti la Yaya Toure likiokolewa na mlinda mlango wakati wa kipindi cha pili.

City-rekodi 3

Draw kwa ajili ya hatua ya robo fainali (nane bora) itapangwa Ijumaa baada ya michezo ya leo kuwa imemalizika (Bayern vs Juventus na Barcelona vs Arsenal)

City-rekodi 4

Pellegrini amesema Kompany anaweza kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kisichopungua miezi minne, kwahiyo City inasubiri kuona kama Otamendi anaweza kurejea uwanjani kwa ajili ya mechi za Premier League dhidi ya Manchester United siku ya Jumapili.

City-rekodi
Rekodi zilizowekwa na Man City
  • Manchester City ni timu ya saba nyingine tofauti kuingia robo fainali ya Champions League kutoka England baada ya Arsenal, Tottenham, Leeds, Liverpool, Manchester United pamoja na Chelsea tangu mwaka 1992
  • Man City wameweka rekodi ya kucheza mechi 10 bila kuruhusu nyavu zao kutikiswa kwenye michuano hiyo ya Ulaya mara ya mwisho ilikuwa ni December 2014 dhidi ya Roma.
City-rekodi 2
  • Mchezo wa jana usiku ulikuwa ni wa pili Manchesyer City inacheza dakika 90 bila kupata bao kwenye michuano ya Champiuons League ndani ya uwanja wa Etihad
  • City waliweza kupiga shuti moja tu on target wkati wa mchezo, shuti hilo lilipigwa dakika ya 73 kipindi cha pili.

 WAKATI HUOHUO;

Atletico

Juanfran alifunga penati ya ushindi kuiwezesha Atletico Madrid kuiondosha PSV Eindhoven kwenye michuano ya Ulaya kwa mikwaju 8-7 na kufuzu hatua ya robo fainali.

Atletico 4

Timu hizo zilishindwa kutambiana katiaka dakika za kawaida 210, ikiwa ni mara ya kwanza kwenye hatua ya mtoano ya Champions League timu kutoka sare ya bila kufngana kwa michezo yote miwili.

Atletico 3

Katika kiwango bora cha upigaji penati, zilishuhudiwa penati 14 zikizama kambani lakini Luciano Narsingh ambaye aliingia dakika za mwisho kuchukua nafasi ya Luuk de Jong, penati yake iligonga mwamba na kushuhudia timu yke kutoka Uholanzi ikiyaaga mashindano.

Rekodi muhimu zilizowekwa kwenye mchezo huo
  • Atletico Madrid ilifanya attempt 26 (pamoja na mashuti yaliyokuwa- blocked) kwenye mchezo huo lakini hawakufanikiwa kufunga goli, ikiwa ni attempt nyingi kufanywa kwenye michuano ya Champions League tangu Sporting Braga walipofanya hivyo dhidi ya Cluj September 2012 (mashuti 38 bila goli)
Atletico 2
  • Jan Oblak ameendelea kuweka rekodi ya kutoruhusu bao langoni kwa Atletico kwenye mashindano yote msimu huu, mechi nyingi zaidi ya golikipa yeyote kutoka ligi tano kubwa za Ulaya msimu huu
Atletico 1
  • Atletico Madrid wamefikisha mchezo wa 13 bila kuruhusu bao kati ya michezo 17 ya Champions League
Atletico 5
  • Hatua ya matuta ilimalizika 8-7, penati nyingi kuwahi kufungwa kwenye historia ya michuano ya Champions League/European Cup

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox