STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 30 Machi 2016

PELE AIJIA JUU KAMPUNI YA SAMSUNG,SASA KUISHTAKI.......



























Mshindi wa kombe la dunia na mwanasoka bora wa muda wote na gwiji wa soka la Brazil Pele, ameifungulia mashtaka kampuni ya Samsung kwa kutumia picha ya sura yake kwenye matangazo ya bidhaa zao bila ruhusa yake.  

 Gwiji huyo wa soka wa Brazil anaishataki kampuni ya Samsung na anaidai fidia ya dola za kimarekani millioni 30 kwa kosa la kampuni hiyo kutumia taswira yake inayofanana na yake katika moha ya matangazo ya bidhaa zao mpya  kwenye  magazeti – bila kuwa na makubaliano nae ya kimkataba, wanaripoti Financial Times .

Tangazo ambalo limeleta mashtaka haya limetokea katika gazeti la The New York Times mwezi Oktoba mwaka jana japo halitoi picha ya moja kwa moja mtu aliyetumika kwenye tangazo hilo ni Pele.. 



  
 Hata hivyo kwa mujibu wa mwanasheria wa mwanasoka huyo amesema picha iliyotumika inayofanana mno na mteja wake pia wameongezea taswira nyingine ya mchezaji akipiga “modified bicycle or scissor-kick, staili ya upigaji mpira ambayo Pele alikuwa akiitumia sana. 

Samsung wamewahi kuwa na mazungumzo na Pele ya kutumia taswira yake tangu mwaka 2013, lakini mazungumzo hayo yalivunjika na Samsung wakokosa haki ya kisheria kutumia taswira ya Pele kwa namna yoyote. 


Mpaka sasa Samsung wamegoma kuzungumzia suala hili walipotafutwa na vyombo vya habari. 


Malalamiko ya Pele yaliyowasilishwa na mwanasheria wake Frederick Sperling yaliongeza – kwamba tangazo la Samsung linaenda kinyume na haki  za kisheria alizonazo Pele – matangazo ya biashara ni sehemu ya kipato anachotegemea mwanasoka huyo mstaafu. 


 
 
Pelé mpaka sasa ana mikataba kadhaa ya kutangaza bidhaa za makampuni kama  Subway, Volkswagen, na Emirates. Kwa maaka 2015 tu alivuna kiasi cha dola million 25. 

Mwanasheria Sperling huko nyuma aliwahi kumsaidia mcheza basketball Micheal Jordan kushinda kesi ya $8.9 million dhidi ya supermarket za Dominick baada ya kumtumia Jordan kwenye matangazo yao bila haki ya kimkataba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox