STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 23 Machi 2016

STARS YATAKATA UGENINI, SAMATA AIBUKA SHUJAA


Mshmbuliaji wa KRC Genk ya Ubelijiji Mbwana Ally Samata ameanza vyema na cheo chake cha unahodha katika timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) baada ya leo kuiongoza stars kushinda goli 1-0 mbele ya Chad.

Samtta leo kwa mara ya kwanza aliiongoza Taifa stars katika mchezo wa kuwania kufuzu kombe la mataifa ya Afrika, mchezo uliochwza katika uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya jijini D'jamena, Chad.
Katika mchezo huo ambao ulianza kwa kasi, goli la Taifa stars lilifungwa na nahodha Mwana Samata katika dakika ya 30 ya mchezo na kupeleka mchezo kumalizika kwa Taifa Stars kuwafunga Chad goli 1-0.

Taifa Stars wanatarajia kurejeana na Chad jumatatu ya marchi 28 katika uwanja wa Taifa ukiwa ni mchezo wa nne wa kun di G, ambapo Stars kwa sasa anafikisha pointi 4.

Kocha wa Taifa stars Charles Boniface Mkwasa amesema vijana wake wamejituma vilivyo hadi kupata ushindi huo kwa kuwa walicheza katika mazingira magumu.

"Hali ya hewa ilikuwa mbaya kabisa lakini vijana wangu walijituma na wanastahili pongezi kabisa," alisema.

"Kipindi cha pili walitushambulia sana, lakini ilikuwa ni lazima kufanya hivyo ili kuhakikisha tunajilinda kuhakikisha hawasawazishi."


Kikosi cha Taifa Stars kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mwinyi Haji Mngwali, Erasto Nyoni, Kevin Yondani, Himid Mao, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto/John Bocco dk46, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu/Ibrahim Hajib dk85 na Farid Mussa/David Mwantika dk73.
 
Chad; Diara Gerard, Abaya Cesar, Kevine Nicaise/Addassou Eli Mathieiu dk50, Nadjim Haroun, Beadoum Monde, Ndounnan Herman, Mahama Azarack, Betolgar Morgan, Djimenan Leger, Ndouassel Ezekiel Na Ninga Casimir. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox