STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 17 Machi 2016

TETESI ZA USAJILI LEO ULAYA, MANU UNITED MBIONI KUMNASA MSHAMBULIAJI WA ARGENTINA

KLABU ya Real Madrid inadaiwa kutarajia kusikiliza ofa kwa ajili ya nyota wake wawili James Rodriquez na Isco majira ya kiangazi ikiwa ni sehemu ya mipango yao kutaka kuimarisha zaidi safu yao ya ushambuliaji.
Chanzo: AS

KLABU ya Arsenal inadaiw akufikiria kumuwania mshambuliaji wa Schalke Roman Neustadter baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kuvunjika. Inter pia nao wanamuwania.
Chanzo: Bild

MSHAMBULIAJI wa Napoli Gonzalo Higuain anadaiwa kukubali mkataba wa miaka mitano na Manchester United baada ya kufanya mazungumzo na Jose Mourinho kuhusiana na uhamisho huo.
Chanzo: Daily Express

MENEJA wa Leicester City Claudio Ranieri anadaiwa kutaka kumpa ofa Francesco Totti ya kucheza soka Ligi Kuu msimu ujao kama ataondoka AS Roma kiangazi hiki.
Chanzo: Fichajes.net

MKURUGENZI wa ufundi wa Barcelona, Robert Fermandez anadaiwa kusafiri kwenda Munich jana kumuangalia Joshua Kimmich wa Bayern Munich ikiwa ni sehemu ya mipango yao ya kutaka kumsajili Javier Mascherano mpya.
Chanzo: Fichajes.net

MENEJA wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino anatarajiwa kuanza mazungumzo ya mkataba mpya na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu. Mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy anataka kumpa kocha huyo mkataba mwingine lakini hawataki suala hilo lisiingiliane na mbio zao za kufukuzia taji la Ligi Kuu.
Chanzo: Evening Standard

KLABU ya Liverpool inadaiwa kujipanga kutoa paundi milioni 10 kwa ajili ya kiungo wa Manchester City Fernando lakini wanakabiliwa na upinzani kutoka kwa klabu ya zamani ya Mbrazil huo ya FC Porto.
Chanzo: The Sun

KLABU ya Manchester City inadaiwa kujiandaa kutoa kitita cha paundi milioni 80 kwa ajili ya kuwasajili Aymeric Laporte na John Stones ili kumpa kocha mpya Pep Guardiola mabeki bora wa kipindi kirefu atakaowahitaji.
Chanzo: Daily Express

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox