STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 31 Machi 2016

YANGA, AZAM ZATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO



YANGA imekata tiketi ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) maarufu kama Kombe la Azam Sports Federations Cup baada ya kuilaza 2-1 Ndanda FC ya Mtwara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/field/image/Azam%20na%20Yanga.jpg?itok=HF-ABnBL
Dakika ya 11 mchezaji wa Ndanda Salvatory Ntebe alikwamisha mpira wavuni akiwa tayari amekwisha otea hali iliyopelekea mzozo na ikamlazimu muamuzi amuonye kwa kadi ya njano kwa kitendo hicho

Yanga walitangulia kupata bao lao dakika ya 27 kupitia kwa mshambuliaji wake, Paul Nonga aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na beki wa kulia Juma Abdul.

Adhabu hiyo ilitolewa baada ya kiungo na Nahodha wa Ndanda, Kiggi Makassy kumchezea faulo mshambuliaji wa Yanga, Mzimbabwe Donald Ngoma nje kidogo ya boksi.

Hadi kipindi cha kwanza kina malizika yanga walikuwa mbele kwa bao moja

Kipindi cha pili, Ndanda walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 56 kupitia kwa Nahodha wake, Kiggi Makassy kwa shuti la nje ya boksi baada ya kuwatoka mabeki wa Yanga.

Baada ya bao hilo, Yanga walicharuka na kufanikiwa kupata bao la ushindi lililofungwa na beki Kevin Patrick Yondan kwa penalti dakika ya 69, baada ya beki wa Ndanda, Paul Ngalema kumkwatua winga Simon Msuva ndani ya boksi.

Ngalema alionyeshwa kadi ya pili ya njano na refa Jimmy Fanuel kwa rafu hiyo na kutolewa nje kwa kadi nyekundu. 
 

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan/Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dk84, Vincent Bossou, Pato Ngonyani/Salum Telela dk58, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Paul Nonga na Deus Kaseke/Godfrey Mwashiuya dk66.

Ndanda FC: Jeremiah Kasubi, Aziz Sibo, Paul Ngalema, Cassian Ponera, Salvatory Ntebe/Ahmed Msumi dk73, Hemed Khoja, William Lucian, Bryson Raphael, Omary Mponda/Salum Minely dk88, Atupele Green na Kiggi Makassy. 
………
Katika mchezo mwingine kwenye mashindano hayo AZAM FC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya kuitandika mabao 3-0 Prisons ya Mbeya jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Azam FC walipata bao lao lao kwanza dakika ya tisa, mfungaji Shomary Kapombe aliyefumua shutibaada piganikupige iliyotokea langoni mwa  Prison.

Kipindi cha pili, Kapombe tena aliifungia Azam FC bao la pili dakika ya 50 akimalizia pasi ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Khamis Mcha ‘Vialli’ aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Nahodha John Bocco, aliipatia Azam FC bao la tatu dakika ya 86.

Azam FC sasa inaungana na Mwadui FC ya Shinyanga iliyoitoa Geita Gold na Yanga iliyoitoa Ndanda FC, wakati Robo Fainali ya mwisho itakuwa kati ya Simba na Coastal Union Aprili 11, Uwanja wa Taifa. 

Kikosi cha Azam FC: Aishi Manula, Shomary Kapombe/Farid Mussa dk80, Waziri Salum/Frank Domayo dk46, Aggrey Morris, Serge Wawa, Erasto Nyoni, Kipre Balou, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Ramadhani Singano ‘Messi’, John Bocco/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk60 na Didier Kavumbagu.

Prisons: Beno Kakolanya, Salum Kimenya, Laulian Mpalile, James Mwosote, Lugano Mwangama,  Jumanne Elfadhil,  Lambarty Sabiyanka/Meshack Suleiman dk62, Freddy Chudu/Baraka Majogoo dk71, Mohamed Mkopi,  Jeremiah Juma/Frank William dk74 na Benjamin Asukile.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox