STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 15 Juni 2016

HILI NDILO KABATI LA MBWANA SAMATTA...............



STRAIKA wa KRC Genk ya Ubelgiji na nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta amekuwa nyota wa Tanzania ambaye amejizolea tuzo nyingi tangu aanze kufahamika. 
 
Mtandao wa BOIPLUS uliamua kumtembelea nyumbani kwake ili kujua anazihifadhi vipi tuzo na medali zote alizowahi kutunukiwa. Hizi hapa ni baadhi ya picha:
Ukifika tu nyumbani kwake utakaribishwa na kabati kubwa lililopambwa kwa medali, vyeti na tuzo mbalimbali alizowahi kutwaa mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba Sc na TP Mazembe ya DR Congo
Licha ya kutisha awapo uwanjani, kumbe Samatta ni mtaalamu wa matumizi ya kiofisi ya kompyuta. Hiki hapa ni cheti chake alichotunukiwa baada ya kuhitimu mafunzo hayo
Mara kadhaa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimekuwa kikimpatia tuzo Samatta kwa kuthamini mchango wake kwenye Tasnia ya michezo nchini, hiki hapa ni cheti alichotunukiwa na TASWA 2015
Katika msimu wa 2013/14, TASWA ilimtaja Samatta kama Mchezaji Bora anayecheza nje ya nchi. Na hii hapa ndio tuzo yake ambayo inapamba kabati lake pia
Mwishoni mwa mwaka jana, Samatta akiwa na TP Mazembe alishiriki michuano ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu huko Japan. Mazembe haikufanya vizuri lakini wachezaji walipewa tuzo za ushiriki ambayo inaonekana hapo juu
TASWA pia ilimpatia tuzo ya Mchezaji mwenye Mafanikio ndani ya miaka 10 kuanzia 2005 hadi 2015
Tuzo nyingine ambayo inapatikana ndani ya kabati la Samatta alipewa na mtandao wa GOAL.COM kama mchezaji bora wa mwaka 2014
2011 akiwa anaitumikia klabu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam alishiriki michuano ya Mapinduzi Cup na kufanikiwa kupata medali ya dhahabu.....nayo ilikutwa imehifadhiwa mahali pake ndani ya kabati
Mwaka jana ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Samatta, licha ya kuvaa medali ya dhahabu ya michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika, mkali huyo wa mabao aliyeanzia soka lake katika viunga vya Mbagala jijini Dar, alifanikiwa pia kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo
Hii ndio tuzo kubwa kabisa ya binafsi aliyowahi kutwaa Samatta, alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Afrika kwa wanaocheza ligi za ndani
Na hiki ni cheti kilichoambatana na tuzo hiyo ya Afrika
2010 Samatta aliungana na vijana wenzake wa Timu ya Taifa ya vijana (U20) huko nchini Eritrea na wakafanikiwa kutwaa medali ya dhahabu katika michuano iliyoandaliwa na CECAFA
Gazeti la michezo la Mwanaspoti lilimtaja Samatta kuwa Mchezaji Bora wa Tanzania anayecheza nje ya nchi. Hiyo ilikuwa katika msimu wa 2012/13
Wengi walimfahamu Samatta akiwa African Lyon ambako alifanya mambo makubwa hadi kuwatamanisha Wekundu wa Msimbazi Simba. Msimu wake wa mwisho akiwa Lyon, Samatta alionyesha uwezo mkubwa ikiwemo kufunga mabao mengi hadi klabu hiyo ikaamua kumtunukia Medali hii maalum
Kwa uzalendo alionao kwa taifa lake, ndani ya kabati hilo Samatta ameweka 'Scarf' ya bendera ya Taifa huku akieleza kuwa anajivunia sana kuwa Mtanzania



Akiwa TP Mazembe, Samatta alifanikiwa kufunga 'Hattrick' tatu, na hii hapa ndio mipira aliyoondoka nayo huko DR Congo. Hata hivyo straika huyo anasikitika kupotelewa na mpira mmoja ambao alikabidhiwa baada ya kupiga Hattrick akiwa Simba SC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox