STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 23 Juni 2016

SIMBA SC YAWACHUKUA KOCHA NA MENEJA WA ZAMANI AZAM FC................



 

KLABU ya Simba inatarajiwa kumtangaza Meneja wa zamani wa Azam FC, Patrick Kahemele kuwa Mtendaji wake Mkuu.

Aidha, Simba inatarajiwa kumtangaza kocha wa zamani wa Azam FC, Mcameroon, Joseph Marius Omog kuwa kocha mpya Mkuu wa klabu hiyo.

 

Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Simba kilitarajiwa kupokea pendekezo la kuajiriwa kwa Kahemele kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu usiku wa kuamkia leo pamoja na Omog kuwa kocha Mkuu.

Na kutokana na Kahemele kuungwa mkono na Wajumbe wengi wa Kamati ya Utendaji, baada ya kazi nzuri aliyowahi kuifanya akiwa Azam FC – kuna matarajio makubwa dili hilo litafanikiwa.

Akizungumza usiku wa jana, Kahemele amesema kwamba amefanya mazungumzo na uongozi wa Simba na kufikia makubaliano, lakini bado hajapewa Mkataba.


 


“Ni kweli, nimefanya mazungumzo na uongozi wa Simba, na kimsingi tumefikia makubaliano ila bado hatujaingia Mkataba,”amesema.


Pamoja na hayo, habari zaidi zinasema Kahemele amewasaidia Simba SC kumpata kocha wa zamani wa Azam FC, Mcameroon Joseph Marius Omog.


“Kahemele ni kiongozi wa kisasa kabisa, mweledi, mchapakazi na mbunifu. Tunaamini atarudisha heshima ya Simba. Hapa hajaanza kazi, lakini ametusaidia vizuri katika mchakato wa kupata kocha,”kimesema chanzo kutoka Simba.


Simba imekuwa haina kocha Mkuu tangu Januari mwaka huu alipoondoka Muingereza, Dylan Kerr mara baada ya kuajiriwa Kocha Msaidizi, Mganda Jackson Mayanja ambaye sasa atafanya kazi chini ya Omog.  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox