STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 28 Juni 2016

YANGA YAAMBULIA KICHAPO MBELE YA MASHABIKI LUKUKI................


 

YANGA SC imevuna matunda ya malumbano badala ya maandalizi kufuatia kufungwa bao 1-0 na TP Mazembe ya DRC katika mchezo wa Kundi A, Kombe la Shirikisho Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
 
Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Yanga, baada ya Juni 19 kufungwa pia 1-0 na wenyeji MO Bejaia 1-0 nchini Algeria.

 
 
Shujaa wa Mazembe leo alikuwa ni Mereveille Boppe aliyemalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki Chrtistian Luyindama dakika ya 74.

 
Katika mchezo huo ambao mashabiki waliingia bure, Mazembe walionyesha kiwango kikubwa zaidi ya Yanga kuashiria kwamba walistahili ushindi huo.








Pamoja na ubora wa Mazembe, lakini leo Yanga ilicheza chini ya kiwango, wachezaji wake wakionekana kabisa kucheza kwa woga na kutojiamini.

 
Shambulizi la maana la Yanga lilikuja dakika ya 44 tu baada ya mshambuliaji Mzimbabwe kufanikiwa kumzidi mbio na maarifa beki Luyindama na kumpasia kiungo Deus Kaseke aliyepiga nje akiwa amebaki na kipa, Sylvain Gbohouo Guelassiognon.

 
Kipindi cha pili, Mazembe walifunguka zaidi na kupeleka mashambulizi mengi langoni mwa Yanga hadi kupata bao lao pekee.


 
 
Kiungo Mzambia, Obrey Chirwa hakuwa na madhara leo, wakati kiungo chipukizi mzalendo Juma Mahadhi alijitahidi ingawa hakuweza kumaliza mechi baada ya kuumia na kumpisha Geoffrey Mwashiuya dakika ya 69.

 
Kuelekea mchezo huo, Yanga ilitumia muda mrefu kulumbana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya matangazo ya Televisheni hadi wakaamua kufuta viingilio siku mbili kabla ya mechi. 


 
 

Yanga itahitimisha mechi zake za mzunguko wa kwanza za Kundi A kwa kucheza na Medeama ya Ghana Agosti 7 Uwanja wa Taifa pia.
 
Vikosi kamili vya leo ni Yanga; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mbuyu Twite, Vincent Bossou, Kevin Yondan, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Juma Mahadhi/Geoffrey Mwashiuya dk69, Obrey Chirwa/Matheo Simon dk71 na Donald Ngoma.

 
TP Mazembe; Sylvain Gbohoud Guelassiognon, Jean Kasusula, Issama Mpeko, Salif Coulibaly, Rodger Asale, Adama Traore/Deogratius Kanda dk76, Merveille Bope, Nathan Sinkala, Koffi Christian/Jose Bodibake dk80, Christian Luyindama na Thomas Ulimwengu.


 grt

MATUKIO MBALIMBALI KABLA YA MCHEZO; 

 Askari Polisi (kushoto) akiwafukuza mashabiki waliojitokeza kuingia bure kwenye mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Yanga na TP Mazembe ya DRC kuondoka baada ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kusheheni watu zaidi ya idadi iliyotakiwa, watazamani 40,000

Askari Polisi akiwa amesimama imara dhidi ya raia ambao bado hawajakata tamaa kuingia uwanjani
Askari zaidi wa Jeshi la Polisi wakipewa mwongozo namna ya kuwadhibiti mashabiki
Raia wakiwa nje ya geti kabla ya kuodolewa kwa mabomu ya machozi
Askari huyu alilazimika kumtandika ngumi shabiki aliyetaka kulazimisha kuingia licha ya kuzuiwa
Uwanja wa Taifa kama unavyoonekana hadi kufika Saa 7:00 mchana 
Mashabiki wa wa wapinzani, Simba wamejitokeza katika nafasi zao ili kuwashangilia wageni, TP Mazembe
Haijulikani sababu ya eneo hili kuachwea wazi. Watu wamezuiwa kukaa hapa

SHUKRANI KWA BINZUBEIRY

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox