STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 6 Septemba 2016

KESSI ATAKIWA KUILIPA SIMBA "MIHELA" KWA KUVUNJA MKATABA



Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Richard Sinamtwa, imemtaka beki wa Yanga, Hassan Kessy kuilipa klabu yake ya zamani, Simba SC shilingi Milioni 120 kwa kuvunja Mkataba.

Kessy ametakiwa kuilipa klabu yake ya zamani, Simba SC kiasi hicho cha fedha ili aanze kuichezea timu yake mpya, Yanga katika mashindano kuanzia sasa.
 Hassan Ramadhani Kessy
Habari za ndani kutoka TFF zimesema kwamba Kamati imejiridhisha kwamba Kessy alivunja mkataba na Simba kinyume cha utaratibu hivyo anapaswa kuilipa Simba.

Habari zaidi zinasema kwamba, katika mkataba wake na Simba, wote klabu na mchezaji walikubaliana atakayevunja mkataba huo atalipa Dola za Marekani 60,000sawa na zaidi ya Shilingi Milioni 120,000 za Tanzania.

Kessy alisajiliwa na Simba SC misimu miwili iliyopita kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa Mkataba wa miaka miwili akilipwa Shilingi Milioni 20.

Naye  Meneja wa Kessy, Athumani Tippo amesema anashangazwa na uamuzi wa Kamati hiyo kumtaka Kessy ailipe Simba.

Tippo amesema mkataba wa Kessy na Simba uliisha tangu Juni 17 na beki huyo wa kulia akasaini Yanga SC Juni 21, baada ya kuzungumzo ya awali kufanyika mwishoni mwa Mei.

“Kilichotokea ni kuwa baada ya habari za Kessy kutaka kuhamia Yanga kuvuja, Mei 25 mwaka huu alipokwenda kwenye mechi ya fainali ya Kombe la TFF dhidi ya Azam mashabiki wakamvisha jezi ya Yanga,” ameongeza.

Amedai kuwa hakuvishwa jezi hiyo na klabu ya Yanga bali ni mashabiki hivyo huwezi kusema Kessy alivunja mkataba na Yanga kinyume cha utaratibu.

Hatahivyo, Meneja  Tippo amesema kwamba amepeleka malalamiko Chama cha Wachezaji Tanzania (SPUTANZA) ili waweze kumsaidia mchezaji huyo katika sakata hilo.

Yanga tayari wameweka msimamo wa kutokuwa tayari kulipa Shilingi Milioni 120 ambazo Simba wanataka ili Kessy aichezee klabu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Jangwani ikimaanisha kuwa kuna uwezekano beki huyo akakaaa jukwaani na kutazama mpira kama shabiki wa Yanga.
Chanzo: Hivi sasa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox