QPR wanalazimika kupokea Pauni Milioni 8.5 na kumruhusu Mchezaji huyo aondoke kama Mkataba wake unavyotaka ikiwa Dau hilo litafikiwa.
Awali ilidhaniwa Arsenal watamchukua Mchezaji huyo ambae ameichezea France Mechi 27 na kufunga Bao 5 lakini sasa inelekea Liverpool wamechukua hatua za haraka kukamilisha Uhamisho wake.
Liverpool, chini ya Meneja wao Brendan Rodgers, tayari wameshanunua Wachezaji wanne kwa ajili ya Msimu mpya ambao ni Adam Lallana, Rickie Lambert, Emre Can na Lazar Markovic.
Kutua kwa Remy Liverpool kutaifanya safu yao ya mashambulizi kuwa mpya ikiwajumuisha Ricky Lambert na Daniel Sturridge baada ya kuwapoteza Luis Suarez alieuzwa Barcelona, Iago Aspas aliepelekwa kwa Mkopo huko Sevilla na Fabio Borini alienunuliwa na Sunderland.
BPL-LIGI KUU ENGLAND
RATIBA MECHI ZA UFUNGUZI
**Saa za Bongo
Jumamosi Agosti 16
14:45 Man Utd v Swansea [Old Trafford]
17:00 Leicester v Everton [King Power Stadium]
17:00 QPR v Hull [Loftus Road Stadium]
17:00 Stoke v Aston Villa [Britannia Stadium]
17:00 West Brom v Sunderland [The Hawthorns]
17:00 West Ham v Spurs [Boleyn Ground]
19:30 Arsenal v Crystal Palace [Emirates Stadiu


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni