STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 1 Septemba 2014

Messi aanza na gundu, yathibishwa ni majeruhi

http://www.barcapakistan.com/wp-content/uploads/2014/01/1388427761_extras_noticia_foton_7_3.jpgNYOTA wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi huenda  akawa nje ya dimba kwa kipindi kifupi baada ya kudaiwa kuumia paja jana wakati wa Ligi Kuu ya Hispania.
Klabu ya Barcelona imetoa taarifa ikidai kuwa nyota wake huyo amepata majeraha ya paja katika mchezo waliopata ushindi mwembamba dhidi ya Villarreal jana
Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo, imedai Messi aliumia msuli wa nyuma ya paja katika mguu wake wa kulia lakini sio majeraha makubwa sana. 
Pia ilithibitisha kuwa mshambuliaji wao mwingine Munir El Haddadi naye aliumia nyama na vipimo vya wote wawili vinatarajiwa kufanyika leo kujua ukubwa wa matatizo ya nyota wake hao. 
Kuna hatari kubwa Messi akakosa mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Argentina na Ujerumani unaotarajiwa kuchezwa keshokuwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox