Kaseja
wao: Kipa wa Uholanzi, Tim Krul akipangua penalti ya nne ya Costa Rica
iliyopigwa na Michael Umana na kuipeleka Uholanzi Nusu Fainali
.
Baada ya timu yake kupelekeshwa kwa dakika 120 na Costa Rica na kushindwa kupata bao, kocha Louis van Gaal alimuingiza kipa wa Newcastle, Tim Krul kwa ajili ya penalti.
Krul alipasha misuli yake moto haraka na kwenda kumbadili Jasper Cillessen dakika ya 118, kisha akaedna kuokoa penalti mbili kuipelekea nchi yake Nusu Fainali ya michuano hiyo.
Krul aliokoa penalti ya pili ya Costa Rica iliyopigwa na mchezaji wa Fulham, Bryan Ruiz na ya nne iliyopigwa na Michael Umana.Raha
zaidi ni kwamba, Nahodha Robin van Persie, Wesley Sneijder, Arjen
Robben na Dirk Kuyt wote wakafunga penalti zao na sasa Uholanzi
itakutana na Argentina katika Nusu Fainali ‘tamu sana’ yenye hadhi hata
ya fainali.
Kikosi cha Uholanzi kilikuwa; Cillessen/Krul, dk120, De Vrij, Vlaar, Martins/Huntelaar dk105, Kuyt, Wijnaldum, Sneijder, Blind, Robben na van Persie, Depay/Lens dk76.
Costa Rica: Navas, Gamboa/Myrie dk78, Acosta, Diaz, Gonzalez, Ruiz, Borges, Tejeda/Cubero dk97, Bolanos, Campbell/Urena dk66 na Umana.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni