KOMBE LA DUNIA: FIFA YAIPA PIGO MARA 2 BRAZIL, MAREFA 15 WABAKISHWA!
Monday, 07 July 2014 19:57
WAKATI
FIFA inawapiga ‘Makonzi mawili’ Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia,
Brazil, Mwenyekiti wa Kamati ya Marefa ya FIFA ametangaza Marefa 15,
kati ya Marefa 25 na Wasaidizi wao, watabaki Brazil na waliobakia kurudi
makwao.
SOMA ZAIDI:
FIFA YAIPA PIGO BRAZIL
LEO FIFA imeitupa Rufaa ya Brazil ya kuitaka ifute Kadi ya Njano ya Nahodha wao
Thiago Silva aliyopewa kwenye Mechi na Colombia na pia imeamua haiwezi
kumchukulia hatua yeyote Beki wa Colombia Juan Camilo Zuniga aliemuumiza
vibaya Mchezaji wa Brazil, Neymar.
Uamuzi
wa kuitupa Rufaa ya Kadi ya Njano ya Thiago Silva unamaanisha Mchezaji
huyo haruhusiwi kucheza Mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Dunia ya
Jumanne Usiku wakati Brazil watakapocheza na Germany.
FIFA imesema hamna mIsingi yeyote ya Kisheria kuikubali Rufaa hiyo.
Kuhusu kumwadhibu Juan Camilo Zuniga,
FIFA imesema haiweza kumchukulia hatua kwa vile Waamuzi wa Mechi hiyo
waliona tukio hilo na kuamua kutochukua hatua yeyote.
MAREFA
Kamati ya Marefa ya FIFA, chini ya
Mwenyekiti wao Jim Boyce, imetangaza kuwa Marefa 15 kati ya 25
waliokuwepo huko Brazil kuchezesha Mechi za Fainali za Kombe la Dunia
wataendelea kubakia Nchini humo na waliobakia wameruhusiwa kurudi
makwao.
Marefa hao 15 ndio wanaoweza kuchaguliwa kuchezesha Mechi 4 za Kombe la Dunia zilizobaki.
Mechi zilizobaki ni Nusu Fainali mbili, Mechi ya kuwania Mshindi wa Tatu na Fainali yenyewe.
Tayari FIFA imemtangaza Refa wa Mexico, Marco RodrÃguez, kuwa ndie Mwamuzi wa Nusu Fainali ya Brazil na Germany.
Miongoni mwa hao 15 waliobaki ni Refa
kutoka England, Howard Webb, mwenye Miaka 42, ambae ndie aliechezesha
Fainali ya Kombe la Dunia ya Mwaka 2010 huko Afrika Kusini ambayo Spain
waliifunga Netherlands Bao 1-0.
Kwenye Fainali hizi za huko Brazil, Webb amechezesha Mechi mbili zile za Colombia v Ivory Coast na Brazil v Chile.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni