
ORODHA KAMILI YA WASHINDI
MCHEZAJI BORA WA AFRIKA - Pierre-Emerick AUBAMEYANG (Gabon)
MCHEZAJI BORA ANAYECHEZA AFRIKA – Mbwana Aly SAMATTA
MCHEZAJI BORA WA KIKE - Gaelle ENGANAMOUIT (Cameroon)
MCHEZAJI BORA KIJANA - Victor OSIMHEN (Nigeria)
MCHEZAJI BORA ANAYECHIPUKIA VIZURI - Etebo Peter OGHENEKARO (Nigeria)
KOCHA BORA WA MWAKA- Herve RENARD (Ufaransa) – Kocha wa zamani wa Ivory Coast
REFA BORA WA MWAKA - Bakary Papa GASSAMA (Gambia)
TIMU BORA YA TAIFA – Ivory Coast
TIMU BORA YA TAIFA YA WANAWAKE- Cameroon
KLABU BORA YA MWAKA - TP Mazembe (DRC)
GWIJI WA AFRIKA - Charles Kumi GYAMFI (Ghana)
Samuel MBAPPE LEPPE (Cameroon)
Kipa: Robert Muteba KIDIABA (DRC)
Mabeki: Serge AURIER (Ivory Coast), Aymen ABDENNOUR (Tunisia), Mohamed MEFTAH (Algeria)
Viungo: Andre AYEW (Ghana), Yaya TOURE (Ivory Coast), Sadio MANE (Senegal), Yacine BRAHIMI (Algeria),
Washambuliaji: Mbwana Aly SAMATTA (Tanzania), Pierre-Emerrick AUBAMEYANG (Gabon), Baghdad BOUNEDJAH (Algeria)
WACHEZAJI WA AKIBA;
Djigui DIARRA (Mali)
Azubuike OKECHUKWU (Nigeria)
Kelechi NWAKALI (Nigeria)
Zinedine FERHAT (Algeria)
Adama TRAORE (Mali)
Victor OSIMHEN (Nigeria)
Kermit ERASMUS (Afrika Kusini)
![]() |
Mbwana Samatta akipokea tuzo yake ukumbi wa mikutano wa kimataifa mjini Abuja |
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Anayecheza Afrika katika sherehe zilizofanyika usiku huu ukumbi wa mikutano wa Kimataifa mjini Abuja.
Samatta
amepata pointi 127, mbele ya mchezaji mwenzake wa TP Mazembe, kipa
Robert Muteba Kidiaba wa DRC, aliyepata pointi 88, wakati mshambuliaji
wa Etoile du Sahel ya Tunisia na timu ya taifa ya Algeria, Baghdad
Bounedjah amepata pointi 63.
Mafanikio
ya Samatta anayeweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo
kubwa ya Afrika, yanakuja baada ya kuiwezesha Mazembe kutwaa taji la
tano la Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akiibuka mfungaji bora kwa mabao
yake nane.
Mshambuliaji wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mara ya kwanza.
Mchezaji bora wa kikeGaelle ENGANAMOUIT
Mchezaji
wa Borussia Dortmund ya Ujerumani mwenye umri wa miaka 26, amewaangusha
Yaya Toure wa Ivory Coast aliyekuwa anashikilia tuzo hiyo na Andre Ayew
wa Ghana.
Amekusanya
pointi 143, saba zaidi ya Toure wakati Ayew ameshika nafasi ya tatu kwa
kupata pointi 112 na anakuwa mchezaji wa kwanza wa
Gabon kushinda tuzo ya CAF
Kiungo wa Nigeria, Etebo Peter Oghenekaro ameshinda tuzo ya Mchezaji Anayechipukia Vizuri dhidi ya Mnigeria mwenzake, Azubuike Okechukwu, kipa wa Mali, Djigui Diarra, Mahmoud Abdelmonem Abdelhamid ‘Kahraba’ wa Misri na Mualgeria, Zinedine Ferhat.
Etebo, anayechezea timu ya Ligi Kuu ya Nigeria, Warri Wolves, aling’ara katika michuano ya U-23 ya Afrika Desemba nchini Senegal, akiibuka mfungaji bora kwa mabao yake matano, yakiwemo mawili aliyofunga katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Algeria katika fainali.
Mshambuliaji
kinda wa Nigeria, Victor Osimhen ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora
Chipukizi akimshinda ndugu yake, Kelechi Nwakali, wachezaji wawili wa
Mali, Adama Traore na Samuel Diarra na Yaw Yeboah wa Ghana.

Osimhen anayeshinda tuzo hiyo siku tisa tangu asherehekee kufikisha miaka 17 ya kuzaliwa, mafanikio hayo yanafuatia kufanya kwake vizuri katika Kombe la Dunia la U-17 Oktoba mwaka jana nchini Chile, akifunga mabao 10 na kuibuka mfungaji bora sambamba na kushinda Mpira wa Fedha baada ya Mchezaji Bora wa pili wa michuano hiyo, huku Nigeria ikitwaa Kombe.
Mfaransa, Herve Renard ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka kwa mara ya pili, baada ya kuipa Ivory Coast ubingwa wa Afrika mwaka jana nchini Equatorial Guinea.

Mfaransa huyo amewashinda Baye Ba wa Mali U-17, Patrice Carteron wa TP Mazembe, Faouzi Benzarti wa Etoile du Sahel na Emmanuel Amunike wa Nigeria U-17.
![]() |
Samatta akiwa na Aubameyang katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa Abuja kabla ya kutangazwa washindi |
Renard, ambaye alishinda tuzo ya kwanza baada ya kuipa Zambia ubingwa wa Afrika mwaka 2012, alikabidhiwa tuzo yake na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Adoum Djibrine.

Cameroon imezishinda Ghana, Afrika Kusini na Zimbabwe katika kipengele cha timu bora ya taifa ya wanawake, wakati Ivory Coast imeziangusha Ghana, Mali U-17, Nigeria U-17 na Nigeria U-23 katika timu bora ya taifa ya wanaume.
Refa
wa Gambia, Papa Bakary Gassama ameshinda tuzo ya refa bora kwa mara ya
pili mfululizo akiwaangusha Ghead Zaglol Grisha wa Misri, Janny Sikazwe
wa Zambia na Eric Arnaud Otogo Castane wa Gabon.

Mualgeria, Haimoudi Djamel pia alishinda tuzo hiyo mara mbili mfululizo mwaka 2012 na 2013.
Kwa mwaka huu wachezaji wote hao waliotajwa hapo juu walipigiwa kura na matokeo ni kama yanavyoonekana kwenye mpangilio hapo chini.
Mbwana Samatta alipata jumla ya kura 127 na hivyo kuongoza, akifuatiwa kwa mbali na mchezaji mwenzie wa TP Mazembe Robert Kidiaba aliyepata kura 88 na aliyefunga Top 3 ni Baghdad Bournedjah. Kura zilipigwa na mataifa 45 ya nchi wanachama wa shirikisho la soka Afrika CAF.
Kwa upande wa Tuzo aliyoshinda Aubemayang kura zilikuwa hivi:
1- @Aubameyang7 143 points
2- @YayaToure 136 points
3- @AyewAndre 112 points
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni