Katika mchezo wa leo Azam FC waliuwanza mchezo kwa kasi na kutengeneza nafasi kadhaa ambazo zilipotea miguuni mwa Kipre Tcheche na Allan Wanga.
Katika dakika ya 20 Kipre Tcheche aliandikia Azam FC goli la pili akiunga kona ya Shomari Kapombe na kuipa uongozi Azam FC.
Kuingia kwa goli hilo kuliongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji wa Azam FC huku wakiendelea kupoteza nafsi za kufunga huku wakiendelea kutawala mchezo.
Katika dakika ya 35 Mafunzo FC walipeleka shambulio lao la kwanza lngoni mwa Azam FC na kufanikiwa kuandika goli la kusawazisha katika dakika ya 35 kupitia kwa Rashid Abdallah.
Kungia kwa goli hilo kuliwarudisha mchezoni Mafunzo na kuanza kutawala eneo la kati na kupelekea Azam FC kuanza kutumia mipira mirefu bila mafanikio yoyote ile na kupelekea kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.
Kipindi cha pili Mafunzo walirejea na kasi ile ile na kutibua mipango yote ya Azam FC huku wakipeleka mashambulizi ya kushtukiza na kupoteza nafsai kadhaaa za kujipatia magoli.
Katika dakika ya 90 mtokea benchi Sadick Rajab aliiandikia Mafunzo goli la pili na kupeleka mchezo kumalizika kwa Mafunzo kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni