
VYOMBO vya habari nchini Ureno, vimeripoti kuwa sanamu la Cristiano Ronaldo lililopo huko Fanchal, mji mkuu wa kisiwa cha Madeira lilivamiwa na wahuni na kupakwa rangi ya jina na namba anayovaa Lionel Messi.
Tukio linadaiwa kufanyika usiku wa kuamkia Jumanne, saa chache baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Agentina na Barcelona kutwaa tuzo yake ya tano ya mchezaji bora wa mwaka wa dunia maarufu kama Ballon d’Or akimshinda Ronaldo.
Jina la Messi pamoja namba 10 zote zilichorwa kwa rangi nyekundu katika sanamu hilo kabla ya wahusika kwenda kusafisha sanamu hilo na kufuta kilichoandikwa.
Akihojiwa dada yake Ronaldo, Katia Aveiro amesema tukio hilo ni la aibu na linaonyesha jinsi wanamuonea wivu ndugu yake huyo.
Ronaldo alizindua sanamu hilo la shaba lenye urefu wa mita 3.40 Desemba mwaka 2014, mita chache kutoka katika makumbusho yake mwenyewe aliyotengeneza katika mji huo.
Wakati huohuo
Kampuni ya Adidas ambao ni wadhamini wa Lionel Messi wamemtengenezea bongo la kiatu.
Adidas
wamemtengenezea Messi kiatu hicho kipya mara tu baada ya kutwaa tuzo ya
tank ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama Ballon d'Or.
Mchezaji huyo mwenye kipaji cha aina yake ameweka rekodi ya kuwa mwanasoka wa kwanza kuchukua tuzo hizo tano.
Cristiano Ronaldo ambaye ni mpinzani wake mkubwa ameendelea kubaki na tuzo tatu.
VYOMBO vya habari
nchini Ureno, vimeripoti kuwa sanamu la Cristiano Ronaldo lililopo huko
Fanchal, mji mkuu wa kisiwa cha Madeira liliamiwa na wahuni na kupakwa
rangi ya jina na namba anayovaa Lionel Messi. Tukio linadaiwa kufanyika
usiku wa kuamkia Jumanne, saa chache baada ya nyota huyo wa kimataifa wa
Agentina na Barcelona kutwaa tuzo yake ya tano ya mchezaji bora wa
mwaka wa dunia maarufu kama Ballon d’Or akimshinda Ronaldo. Jina la
Messi pamoja namba 10 zote zilichorwa kwa rangi nyekundu katika sanamu
hilo kabla ya wahusika kwenda kusafisha sanamu hilo na kufuta
kilichoandikwa. Akihojiwa dada yake Ronaldo, Katia Aveiro amesema tukio
hilo ni la aibuna linaonyesha jinsi wanamuonea wivu ndugu yake huyo.
Ronaldo alizindua sanamu hilo la shaba lenye urefu wa mita 3.40 Desemba
mwaka 2014, mita chache kutoka katika makumbusho yake mwenyewe
aliyotengeneza katika mji huo.
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni