BEKI wa zamani wa
Arsenal, Kolo Toure amesema Uwanja wa Emirates ndio chanzo kikubwa cha
klabu hiyo kushindwa kunyakuwa taji la Ligi Kuu katika kipindi cha miaka
10 iliyopita.
Arsenal walikuwa wakitumia Uwanja wa Highbury kabla ya
kuamua kujenga uwanja mpya wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 ambao
walihamia mwaka 2006.
Taji la mwisho la ligi kuchukuliwa na Arsenal
ilikuwa msimu wa 2003-2004 wakati klabu hiyo ilipomaliza msimu bila
kufungwa na wamenyakuwa mataji manne pekee toka wakati huo.
Lakini Toure
amempongeza meneja wa timu hiyo Wenger kwa juhudi zake toka wakati huo
baada ya klabu kulazimika kupunguza matumizi kwa miaka kadhaa ili kuweka
mahesabu yao sawasawa.
Toure amesema ingawa hayuko katika klabu hiyo
lakini kuna mambo mengi yalibadilika, wachezaji wengi waliondoka akiwemo
Patrick Vieira hivyo iliwawia vigumu lakini sera hiyo ilianza wakati
wameanza ujenzi wa uwanja mpya.
Toure aliendelea kudai kuwa Arsenal
ililazimika kuuza nyota wake akiwemo Robert Pires, Thiarry Henry na
kulazimika kuanza kutegemea wachezaji chipukizi wasiokuwa na uzoefu
wowote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni