PRESS RELEASE
TAREHE 5 JUNI 2015
YAH: MGOGORO KATI YA MCHEZAJI RAMADHAN SINGANO NA KLABU YA SIMBA.
TFF imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya Mchezaji Ramadhani Singano wa klabu ya Simba.
TFF
imeagiza mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Simba
wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne tarehe 09/06/2015 kwa mazungumzo.
Kila upande umetakiwa uje na vielelezo vyake.
Katika
kipindi hiki cha kuelekea kwenye mazungumzo,TFF inaziasa pande zote
mbili zijiepushe na kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya
kutoelewana na kuamsha hisia mbaya katika familia ya mpira wa Miguu
Tanzania.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni