Klabu hiyo ya meneja Arsene Wenger inaikaribisha Besiktas ya Uturuki katika mechi ya marudiano ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa
Ulaya, Ze Gunnerz wakihitaji ushindi ili kuingia kwenye makundi.
Katika mechi ya mkondo
wa kwanza timu hizo zilipokutana mjini Instabul, zilishindwa kutambiana
baada ya kutoka sare ya bila magoli, huku Arsenal ikimpoteza nyota wake
kwa kupewa kadi mbili za njano na kufuatia nyekundu.
Walshere anaamini Arsenal wapo poa baada ya kufanikiwa kutoka nyuma kwa kufungwa mabao
2-0 na kufanikiwa kutoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Everton Jumamosi
iliyopita.
Akihojiwa Wilshere
amesema alama waliyopata dhidi ya everton
ilikuwa ni muhimu kwani inawapa nguvu kwa ajili ya mchezo wao wa leo
ambapo sare ya aina yoyote inaweza kuwaondoa mashindano ikiwa ni mara ya
kwanza baada ya miaka mingi kwa vijana hao wa Emirates.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni