STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 30 Agosti 2014

BREAKING NEWS; SIMBA YAMTEMA MOSOTI, YASAJILI KINDA LA ZANZIBAR HEROES


 Donald Mosoti (katikati) ametemwa. Kulia ni kocha Mcroatia Zdravko Logarusc aliyetimuliwa na kushoto kipa Ivo Mapunda, ambao kwa pamoja watatu hao walijiunga na Simba SC Desemba mwaka jana kutoka Gor Mahia ya Kenya

SIMBA SC imefikia uamuzi wa kumtema beki Mkenya, Donald Mosoti na kumsajili beki chipukizi wa timu ya taifa ya Zanzibar, Shaffi Hassan ambaye msimu uliopita aliichezea Ashanti United katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

.
Beki huyo wa kati kinda aliyekuwa akimuweka benchi mkongwe Vicotr Costa mbele ya kocha mkongwe, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ amesaini Mkataba wa miezi sita jana visiwani Zanzibar.
Jana hiyo hiyo jina lake limetumwa kwenye usajili wa Simba SC na kuwahi kabla ya dirisha kufungwa.
Hatua ya Simba SC kumkata beki huyo mrefu inafuatia kumsajili mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi ambaye klabu yake, Yanga SC inadai haijamuacha na bado ina mkataba naye. 
Simba SC imelazimika kukata mgeni mmoja, Mosoti ili ibaki na wachezaji watano wa kigeni kwa mujibu wa kanuni baada ya kumsajili na Okwi. Wengine ni Mganda, Joseph Owino, Warundi, Pierre Kwizera na Amisi Tambwe na Mkenya, Paul Mungai Kiongera.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox