STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 19 Agosti 2014

KISANGA CHA AJABU UFARANSA: MARSEILLE WALILAZIMIKA KUMTOA UWANJANI ANDRE AYEW BAADA YA KUKOSA JEZI YA KUMVALISHA!

507046161XL025_OLYMPIQUE_DEMARSEILLE walifungua vibaya uwanja wa Stade Velodrome baada ya kuchapwa na wageni Montpellier.
Rais wa UEFA, Michel Platini alikuwepo katika uwanja huo, lakini ni mechi ambayo wenyeji kamwe hawataisahau.
Kupoteza mabao 2-0 dhidi ya Montpellier yalikuwa matokeo mabaya na hali ya kisanga cha Andre Ayew kilibaki kuwa gumzo uwanjani.
Nyota huyo wa Ghana katika fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil,  alipata majeraha kichwani kipindi cha kwanza na ilimlazimu kubadilisha jezi baada ya damu kutawala katika jezi yake na
aliendelea na mechi.
Kipindi cha pili, bandeji katika jeraha hilo ilitoka na damu kuanza kutoka na kuchafua jezi yake na ikambidi abadili tena. Lakini kulikuwa na tatizo.
Marseille walikuwa na jezi zake mbili tu namba 10 mgongoni na yatari alikuwa ameshazichafua zote kwa damu.
(Screencap thanks to Alex Baker)

Ayew alionekana katika TV ya uwanjani akiwa amechukizwa na kitendo hicho
Mtunza vifaa wa klabu hiyo alitoa jezi namba 33, lakini kwa kuwa Ayew alianza mechi kwa kuvaa jezi namba 10, alitakiwa kumaliza mechi kwa namba hiyo hiyo.
Kwahiyo, timu ilijaribu kufuta namba 33 na kuandika namba 10, lakini jitihada ziligonga mwamba, kwahiyo Marseille ikabidi wamtoe Ayew katika dakika ya 52 baada ya kukosa jezi. Hali hii ilimchefua sana kocha Marcelo Bielsa.
Hakuna aliyemtia moyo, Ayew alirudi benchi akiwa hana jezi yoyote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox