STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 29 Agosti 2014

Samuel Eto'oo afunguka 'Sina bifu na Mourinho'

MSHAMBULIAJI mpya wa Evetrion, Samuel Eto'o ametupilia mbali madai kuwa ana bifu na Jose Mourinho wakati timu yake ikijiandaa kuivaa Chelsea katika mechi ya Ligi Kuu ya England kesho Jumamosi.
 
Eto’o, Mchezaji wa Kimataifa wa Cameroon, na Meneja wa Chelsea Jose Mourinho walikuwa pamoja huko Inter Milan na kutwaa UEFA
CHAMPIONS LIGI pamoja na akaja England Mwaka mmoja uliopita kuungana na Mourinho huko Chelsea.
Lakini uhusiano wa Eto’o na Mourinho ulipata msukosuko pale Mreno huyo aliponaswa kwenye Kamera bila kujijua akidhihaki Umri wa Eto’o na kudai ni Mzee kupita Miaka inayodaiwa anayo. Mara baada ya tukio hilo Eto’o, mwenye Miaka 33, alifunga Bao akiichezea Chelsea na kwenda kushangilia mithili ya Mzee akishika Kibendera cha Kona kama Mkongojo huku akijishika Kiuno ili kumdhihaki Mourinho.
Akiongea na Wanahabari mara tu baada ya kutambulishwa kama Mchezaji mpya, Eto’o alipuuza madai hayo ya kuwa na bifu na Mourinho na badala yake kusema anamshukuru Mourinho kwa kumleta Ligi Kuu England.

Nae Meneja wa Everton Roberto Martinez amedokeza kuwa huenda Mkongwe huyo wa Cameroon akaivaa Chelsea Jumamosi wakati watakapopambana Goodison Park katika Mechi ya Ligi Kuu England.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox