STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 10 Agosti 2014

TETESI ZA USAJILI BARAN ULAYA KWA MUJIBU WA MAGAZETI YA LEO TAREHE 10



Manchester United wametoa dau la pauni milioni 55 kumtaka kiungo wa Real Madrid Angel Di Maria, 26 (Daily Express), United pia watatazama kumchukua kiungo wa zamani wa Arsenal Alex Song, 26, kutoka Barcelona iwapo watashindwa kumpata Arturo Vidal, 27 (Daily Express),

Salim Kikeke's photo.
 Borussia Dortmund wamesema watafanya kila wawezalo kubaki na kiungo wao Marco Reus, 25, licha ya mchezaji huyo kuwindwa na Arsenal, Liverpool na Manchester United (Metro), Manchester City wapo karibu kukamilisha usajili wa beki wa Porto Eliaquim Mangala, 23 kwa kitita cha pauni milioni 32 (Daily Mail), beki wa kushoto wa Sevilla Alberto Moreno, 22, atakamilisha uhamisho wake kwenda Liverpool wiki ijayo, baada ya kucheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Real Madrid katika michuano ya Uefa Super Cup, jijini Cardiff (Daily Mirror), Atletico Madrid wanataka kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Roberto Soldado, 29, kwa mkopo, lakini Spurs wangependa kumuuza kabisa (Daily Telegraph), Tottenham wanamfuatilia winga kutoka Nigeria Moses Simon, 19 anayechezea Trencin (Daily Mirror), Everton wamekubaliana na Chelsea kumchukua Christian Atsu, 22 kwa mkopo (Daily Mail), Real Madrid wanajiandaa kutoa pauni milioni 10 kumchukua kipa, Petr Cech (Daily Express), wakala wa winga wa Fiorentina Juan Cuadrado atasafiri kwenda England weekend hii ili kuzungumza na Manchester United juu ya mkataba wa pauni kati ya milioni 30 hadi 35 (Marca), Liverpool watamfuatilia Ezequiel Lavezzi baada ya PSG kumwambia mshambuliaji huyo kuwa atauzwa (Daily Express)
.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox