STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 13 Septemba 2014

HAPANA CHEZEA VIPERS FC! WAICHAPA MBEYA CITY 4-1 SOKOINE

Na Baraka Mpenja
WAGONGA nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc wametandikwa mabao 4-1 na Vipers FC (Zamani Bunamwaya) inayoshiriki ligi ya Uganda katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyomalizika jioni ya leo uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Vipers FC waliowasili leo asubuhi jijini humo walitandaza soka safi na kuwazidi wenyeji wao karibia idara zote.
Hata hivyo taarifa kutoka kwa shuhuda wetu aliyekuwepo uwanjani hapo, Mbeya City walijitahidi kugangamala, lakini walionekana kutokuwa na ushindani wa ngazi ya kimataifa.
Mechi hiyo ni ya mwisho ya kujipima ubavu kwa kocha Juma Mwambusi ambaye  ana changamoto ya kufanya vizuri katika msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajia kuanza kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu.
Mwambusi aliyeibuka kuwa kocha bora msimu uliopita, anasaidiwa na Suleiman Jabiri baada ya msaidizi wake Maka Mwalwisyi kukataa kuongeza mkataba muda mfupi baada ya ligi kuu msimu uliopita kumalizika.
Maka kwasasa ni kocha mkuu wa klabu ya Panone FC ya mkoani Kilimanjaro na inashiriki ligi daraja la kwanza.
Mbeya City msimu uliopita walimaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na mabingwa Azam fc.

Wakali hao wanaovalia jezi za zambarao wataanza kampeni ya ligi kuu msimu wa 2014/2015 kwa kuwakaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, septemba 20 mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox