STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 13 Septemba 2014

SIMBA YAKALIWA KOONI NA NDANDA FC, YATOKA 0-0 NANGWANDA SIJAONA MTWARA

Kikosi cha Simba kilichoanza leo dhidi ya Ndanda fc uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara

Na Baraka Mpenja
SIMBA SC chini ya kocha Mzambia, Patrick Phiri imeshindwa kutamba mbele ya Ndanda fc na kutoka suluhu pacha ya bila kufungana (0-0) katika mchezo wa kirafiki uliopigwa jioni hii uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Hii ni mechi ya pili kwa Simba ndani ya saa 24 ambapo jana uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ilifungwa bao 1-0 na URA ya Uganda katika mechi ya kimataifa ya kirafiki.
Kabla ya hapo, Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, wikiendi iliyopita uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mshambuliaji Mkenya, Paul Kiongera alifunga mawili na Ramadhani Singano ‘Messi’ alifunga moja.
Katika mechi hizo mbili za kimataifa, Mfungaji bora wa msimu uliopita, Mrundi, Amissi Tambwe hakucheza, lakini leo alianzishwa na kocha Phiri, ingawa alishinda kuziona nyavu.
Kikosi cha Ndanda fc kilichoanza dhidi ya Simba sc

Kwa ujumla mechi ya leo huko Mtwara ilikuwa nzuri na vijana wa Ndanda walicheza kwa kiwango kizuri, hivyo kuwa kipimo sahihi kwa Simba sc.
Simba nao walionesha soka zuri na kuifanya mechi kuwa 50-50, lakini hawakuwa na ujanja wa kuwafunga Ndanda fc walioshuhudiwa na umati mkubwa wa mashabiki wao.

Uwanja wa Nangwanda ulifurika mashabiki ambao walikuwa na hamu ya kuiona Simba ikiwa ni miaka mingi imepita bila kuona klabu kubwa ya ligi kuu ikicheza mkoani humo.
Simba walicheza mbele ya Rais wao, Evans Elieza Aveva ambaye jana aliongozana na mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Hassan Dalali kuzindua tawi la Simba mkoani Mtwara.
Rais wa Simba sc, Evans Elieza Aveva (wa kwanza kushoto, wanaotembea) akiingia Jukwaa kuu

Mechi hii ni ya mwisho ya majaribio kwa kocha Phiri na kikosi chake kinarejea Dar es salaam kabla ya kurudi tena kambini Visiwani Zanzibar kumalizia program ya maandalizi yake.
Simba wataanza ligi kuu septemba 21 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa kuwakabili wagosi wa Kaya, Coastal Union.
Wakati wao Ndanda fc watasafiri mpaka uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga kuwavaa wenyeji Stand United, septemba 20 mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox