STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 7 Septemba 2014

LOIC REMY: BADO SIELEWI KWANINI SIO MCHEZAJI WA LIVERPOOL...LAKINI NINA FURAHA KUWA CHELSEA

Setback: Loic Remy was set to move to Liverpool before the Reds pulled out of the deal
Tatizo: Loic Remy  alikaribia kusajiliwa Liverpool kabla ya dili kushindikana.

MSHAMBULIAJI wa Chelsea,  Loic Remy amesema bado haelewi kwanini dili la kujiunga na Liverpool majira ya kiangazi lilivunjika.
Nyota huyo mwenye miaka 27 alitazamiwa kujiunga Anfield kwa dau la paundi milioni 8 kabla ya wekundu hao kulitupilia mbali dili hilo wakidai mchezaji huyo ameshindwa kufuzu vipimo vya afya.
Remy alishindwa kufuzu vipimo vya afya kutokana na matatizo ya moyo na goti, lakini alishangazwa na tangazo hilo.
"Binafsi sikuelewa. Tatizo wakati wa vipimo vya afya? sijui. Walitengenezea, lazima itakuwa hivyo," aliwaambia Daily Star.
Mfaransa huyo alirejea QPR na alionekana katika mechi ya ligi kuu kabla ya kujiunga na Chelsea wiki ya mwisho ya usajili ambapo atacheza kumsaidia Diego Costa ambaye amepata majeraha ya nyama za paja katika majukumu ya kimataifa.
Delight: Remy signed for Chelsea on final week of the transfer window
Furaha: Remy alitua Chelsea  wiki ya mwisho ya usajili.

Remy, ambaye aliifungia Ufaransa bao la ushindi dhidi ya Hispania siku ya alhamisi, alisema; "Kichwani mwangu, nilitaka kuendelea kukaa QPR, lakini sikuogopa kwa sababu nyingi  nilizonazo: Kwa jinsi nilivyojiimarisha, kujiamini kwangu na kwa namna Chelsea walivyonihitaji, nilikubali kwasababu hii ni moja ya klabu kubwa duniani.
"Nina furaha ya kujiunga na klabu hii"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox