Wayne
Rooney amewaomba radhi Wachezaji wenzake kwa kutolewa nje kwa Kadi
Nyekundu kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Jumamosi huko Old Trafford
wakati Manchester United inaifunga West Ham.
Rooney
alipewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 54 na Refa Lee Mason kwa
kumchezea Rafu Stewart Downing na amesema hana mpango wa kukata Rufaa.
Kutokana
na Kadi hiyo, Rooney atazikosa Mechi 3 za Ligi ambazo ni dhidi ya
Everton, WBA na Chelsea na atarejea Uwanjani Novemba 2 kwenye Dabi ya
Jiji la Manchester dhidi ya Man City kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Kuhusu Kadi hiyo, Bosi wa Man United, Louis van Gaal, alikiri kuwa ilistahili kwani alikosea jinsi ya kumsimamisha Downing aliekuwa akichanja mbuga .
Mwenyewe
Rooney ameeleza: “Nilimwona Mchezaji wa West Ham akifanya kaunta ataki
na mimi nilijaribu kuvunja hiyo lakini nilikosea namna ya kumzuia.
Nimefarijika wenzangu walilinda Bao zetu na tumeshinda.”
Kuhusu Kadi hiyo, Bosi wa Man United, Louis van Gaal, alikiri kuwa ilistahili kwani alikosea jinsi ya kumsimamisha Downing aliekuwa akichanja mbuga .


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni