Kocha
wa timu ya Taifa ya Benin, Olle Didier Nicolle ametaja kikosi cha
wachezaji 18 kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa
Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mfaransa
huyo ameita wachezaji 13 wanaocheza nje ya nchi hiyo akiwemo kiungo
Stephane Sessegnon wa West Bromwich Albion ya Uingereza kwa ajili ya
mechi hiyo ya Kalenda ya FIFA itakayoanza saa 11 jioni.
Katika picha ni Stephane Sessegnon, kiungo mshambuliaji wa Bernin ambaye atakuwepo katika kikosi kitakacho kabiliana na Stars.
Kwa mujibu wa rekodi zilizopo katika mtandao wa klabu yake ya West Bromwich Albion, zina onyesha kwamba, jamaa hana kasi lakini ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. |
Wachezaji
wengine katika kikosi hicho ni Didier Sossa (AS Dragons FC de I’Oueme,
Benin), Abdel Fadel Suanon (Etoile Sportive du Sahel, Tunisia), Jodel
Dossou (FC Liefering, Austria), Sessi D’almeida (FC Girondis Bordeaux,
Ufaransa), Mohamed Aoudo (JS Saoura, Algeria) na Saturnin Allagbe (US
Krake, Benin).
Steve
Mounie (HSC Montpellier, Ufaransa), Farnolle Fabien (Clermont Foot
Auvergne 63, Ufaransa), Jordan Adeoti (SM Caen, Ufaransa), Michael Pote
(Omonia Nikosia, Cyprus), David Djigla (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa)
na Seidou Baraze (Kawkab Marrakech, Morocco).
Jean
Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club, Benin), Nafiou Badarou (ASO Chlef,
Algeria), Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin), Fortune Ore (US
Krake, Benin) na Seibou Mama (US Krake, Benin).
Msafara
wa timu hiyo utaanza kuingia nchini kesho (Oktoba 9 mwaka huu) kwa
nyakati tofauti, na utakuwa umekamilika (Oktoba 10 mwaka huu). Timu hiyo
itafikia hoteli ya JB Belmont.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni